HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2020

VETA YALETA MASHINE YA KUCHAKATA UBUYU

Mwalimu wa Mamlaka ya Elimu a Ufundi Stadi  (VETA) Morogoro na Mbunifu wa mashine ya kuchakata ubuyu , Fredrick Uliki akionesha mashine hiyo.


Na Janet Jovin

MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), imesema kuwa katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba kwa mwaka huu, imeleta mashine maalum ya kuchakata ubuyu ambayo inaelezwa kuwa itakuwa mkombozi kwa wauzaji wa unga wa ubuyu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika banda la mamlaka hiyo lililopo kwenye maonesho hayo, Mwalimu wa VETA Morogoro na Mbunifu wa mashine hiyo, Fredrick Uliki anasema wazo la kutengeneza mashine alilipata baada ya kufanya utafiti kwa wakulima ambao utumia mikono kitenganisha mbegu za ubugu na unga wake.

Anasema alibaini kuwa wakulima hao ambao wengi wao ni wanawake utumia muda mwingine kupata unga hivyo akaamua kutengeneza mashine hiyo ambayo ilimchukua zaidi ya miezi sita kuweza kuikamilisha.

"Nilitumia miezi sita kukamilisha mashine hii kwa sababu nilikuwa natengeneza na kubomoa kutokana na kutofanya kazi vizuri, ndipo nikafanikiwa kuipata hii ambayo inawalenga kinamama na katika kila dakika 3 uchakata kilo 25 za ubuyu," anasema.

Anasema kutokana na uzalishaji wa mashine hizo kwa sasa kuwa mdogo,  gharama ya mashine moja  ni sh. Milioni tatu.

Hata hivyo anasema licha ya mibuyu kupatikana kwa wingi katika maeneo mbalimbali na unga wake kuwa na manufaa mengi, bado haijaweza kuwanufaisha wananchi wengi kiuchumi.

Anasema hiyo ni kutokana na ugumu wa uziduaji wa unga wa ubuyu kwa matumizi mapana ya jamii.

"Njia zinazotumika kuzidua ni za kiasili, kama kutwanga ambazo huharibu ubora wa unga na huwa hazina ufanisi wa kiwango kikubwa, wengine huloweka kwenye maji kisha kukausha jambo ambalo linapunguza baadhi ya virutubisho na ubora wa unga kwa ujumla," anasema.

No comments:

Post a Comment

Pages