Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ametembelea
banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020
yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika banda la Wizara
Dkt. Ndumbaro amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa
zaidi ili kuiletea sifa Serikali na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kimataifa.
"Kwa kuwa sisi
tunafanya kazi ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nje na kuhakikisha mahusiano
ya kimataifa yanaimarika hatuna budi kufanya kazi kwa bidii na maarifa yetu
yote, hili ni jukumu letu hivyo ni lazima tuhakikishe tunalitekeleza kwa
ufanisi na ufasaha," Amesema Dkt. Ndumbaro
Akiwa katika maonesho ya 44
ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Dkt. Ndumbaro ametembelea pia banda la Bunge,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania.
Watumishi wa Wizara
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, alipotembelea banda la Wizara katika maonesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dkt. Ndumbaro, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika maonesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment