HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 27, 2020

Lissu atua nchini, wafuasi Chadema wamshangilia

Wafuasi wa Chadema wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lissu.
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakimlaki Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu.


Na Janeth Jovin


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu ameshawasili Tanzania akitokea nchini Ubelgiji alipokaa takribani miaka mitatu akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017.

Hata hivyo maelefu ya wanachama waliojitokeza kumpokea kiongozi huyo wa chama cha upinzani walipomuona walianga kupiga kelele na kumshangilia.

Lissu amewasili leo katika Uwanja vya Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 7:45 na ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Hata hivyo baada ya Lissu kuwasili maelfu ya wafuasi wa Chadema waliojitokeza kumpokea walimshangilia kwa kuanza kuimba ‘Rais rais rais huyooo, rais huku wakianza msafara wa kutoka uwanjani hapo kwenda Ofisi za Makamu Makuu ya Chadema, mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wafuasi hao wa Chadema waliokuwa wakiimba nyimbo hizo kila mmoja alitaka kumsogelea Lissu lakini kutokana na ulinzi ulioimarishwa walishindwa kumshika wala kumsogelea kwa ukaribu.

Lissu alipigwa risasi katika makazi yake Area D jijini Dodoma na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa matibabu.

Usiku huohuo alisafirishwa akiwa hajitambui kwenda Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi hadi tarehe 6 Januari 2018 alipohamishwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi

No comments:

Post a Comment

Pages