Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameondoka Ofisi za Makao Makuu kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), tayari kwa kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa (Bara), Tundu Lissu.
Hata hivyo mamia kwa maelfu ya wafuasi wa chama hicho wajitokeza kwa wingi katika uwanja huo wa ndege kumpokea Lissu.
Lissu anatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Saa 7.20 mchana huu.
Baada ya kupokelewa JNIA, Makamu Mwenyekiti huyo ataelekea Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, jijini Dar es Salaam, ambapo atazungumza na Waandishi wa Habari.
Kadri muda unavyokwenda, viongozi na wanachama wa Chadema wanamiminika uwanjani hapo ili kumpokea Lissu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho anayetarajia kutua saa 7:20 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
Miongoni waliofika kumpokea ni, Alute Mughwai, kaka yake na Vicent ambaye ni mdogo wake.
Pia, waliokuwa wabunge wa chama hicho, John Heche (Tarime Vijijini), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Mbeya Mjini), Godbless Lema (Arusha Mjini), mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai na aliyekuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob
No comments:
Post a Comment