Na Makuburi Ally
MWANADADA Radhia Japhet Solomon mwenye mapacha wanne amejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania ubunge viti maalum Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Radhia ni mmoja wa wagombea zaidi ya 180 waliojitokeza katika mchakato huo tangu Julai 14.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule Wanawake wameonesha kwamba wanaweza kutekeleza majukumu ya jamii kwa sababu hawajawahi kushindwa katika nafasi wanazopewa.
Haule alisema kujitokeza kwa idadi kubwa ya wagombea zaidi kumetokana na hamasa waliyoifanya kuanzia ngazi ya matawi Kata Wilaya Mkoa na Taifa.
Naye Radhia alisema amejitokeza kuchukua fomu baada ya kujipima na kujiona kwamba anatosha kuitumikia nafasi hiyo.
Radhia
Japhet Solomon mwenye mapacha wanne akipokea fomu ya kuwania ubunge viti maalum Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
Radhia
Japhet Solomon mwenye mapacha wanne, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge viti maalum Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
Radhia
Japhet Solomon mwenye akiwa na mapacha wake.
No comments:
Post a Comment