Naibu Waziri wa
Maliasili, Constantine Kanyasu, akizunguma na Meneja wa Shamba la
Miti Sao Hill pamoja na Afisa Misitu Glory Fortunatus ( wa kwa kushoto)
wakati akiangalia miti iliyooteshwa kwa vifaa maalumu ambayo ipo tayari
kwa ajili ya kupelekwa shambani kwa ajili ya kupandwa. (Picha na Wizara ya Malasili na Utalii).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu, akiwa
ameongoza na Watumishi wa Shamba laMiti la Sao Hill akipewa maelezo na
Afisa Misitu, Glory Fortunatus wakati alipokuwa akitembelea bustani ya
miti ya shamva hilo lililopo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Na Mwandishi Wetu
Ameyasema
hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Shamba la Miti
la Sao Hill linalosimamiwa na TFS lililopo katika wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa
Amesema
eneo hilo la ardhi lenye mgogoro lina ukubwa wa hekta 1705 ambazo kati
ya hizo hekta 600 zilishapandwa miti na TFS ila baada ya mgogoro huo
kuibuka kila Taasisi ikidai kuwa eneo hilo ni lake ilipelekea TFS
kushindwa kumalizia kupanda miti katika eneo lililokuwa limebaki lenye
jumla ya hekta 800.
Kufuatia hali hiyo, Mhe.
Kanyasu ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo
ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ishughulikie mgogoro huo uliopo baina ya
JKT Mafinga na Shamba la Miti Sao Hill ili kila Taasisi ijikite kwenye
majukumu yake ya msingi.
"
Mgogoro huu usipotafutiwa ufumbuzi wa haraka utaleta athari, Kitendo
cha JKT Mafinga kung'oa vigingi vilivyowekwa na TFS kwa ajili ya
kubainisha mipaka haileti picha nzuri ikizingatiwa kuwa zote hizo ni
Taasisi za Serikali" alisisitiza.
Amesema
endapo Kamati hiyo Ulinzi na Usalama itafika mwisho na kushindwa kupata
majibu juu ya mgogoro huo imshirikishe Mkuu wa mkoa wa Iringa ili
mgogoro huo uweze kuisha.
Amesema
ni lazima mgogoro huo ufike mwisho na ikishindikana Mkuu wa Mkoa
ashirikishwe hali itakayosaidia kuleta suluhu ya kudumu na kuzifanya
Taasisi hizo kuendelea kutoa huduma kwa jamii badala ya kuendelea
kusigana kila kukicha.
" Nina amini Mkuu wa mkoa ana vyombo na. uwezo wa kumaliza mgogoro huu kwa vile hizi zote ni Taasisi za Serikali" alisisitiza Mhe.Kanyasu
Hata
hivyo, Mhe.Kanyasu amesema endapo Mkuu wa Mkoa atashindwa kuutafutia
majibu mgogoro huo basi aitaarifu Wizara ya Maliasili na Utalii ili
iweze kukutana Wizara husika kwa lengo la kumaliza mgogoro huo.
Amesema
anataka mgogoro huo ufike mwisho na kama nyaraka zitaonesha kuwa eneo
hilo la JKT basi JKT wapewe na kama ikithibitika ni eneo hilo ni mali ya
TFS wapewe ili waweze kupanda miti.
"
Jukumu letu sisi ni kupanda miti tunachotaka ni kuona eneo hilo
linapandwa miti bila kujali kapanda nani JKT au TFS " alisisitiza
Mhe.Kanyasu.
Hata
hivyo, Mhe.Kanyasu amempongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuushughulikia
mgogoro huo licha ya kuwa umekuwa ukienda taratibu sana na hivyo kasi ya
TFS kumalizia kupanda miti katika eneo hilo imekuwa ikitatizwa na
kuwepo kwa mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment