Wanafunzi wa
Sekondari ya Wavulana ya Oswe wakimtazama Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akiwachapa viboko nane mwanafunzi wa shule hiyo waliochoma
moto mabweni ya shule hiyo Julai 3 Mwaka huu na kusababisha hasara ya Zaidi ya
shilingi milioni 26.
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela Mapema leo akimchapa viboko nane
mwanafunzi wa kidato cha Pili wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Oswe kwa
kutotoa taarifa alizozifahamu kuhusu mpango wa kuchomwa moto mabweni ya shule
hiyo Julai 3 Mwaka huu na kusababisha hasara ya Zaidi ya shilingi milioni 26.
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela Mapema leo akimchapa viboko nane mwanafunzi Naftari Nganga wa kidato cha Pili wa shule ya sekondari ya Wavulana
ya Oswe kwa kuchoma moto mabweni ya shule hiyo Julai 3 Mwaka huu na kusababisha
hasara ya Zaidi ya shilingi milioni 26.
Songwe, Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela mapema leo amewachapa viboko wanafunzi
watano waliohusika katika tukio la kuchoma moto shule ya sekondari ya Wavulana
ya Oswe na kusababisha hasara ya Zaidi ya shilingi milioni 26.
Brig. Jen. Mwangela
amefikia hatua hiyo mara baada ya kamati aliyoiunda ya kuchunguza chanzo cha
ajali ya moto uliotokea shuleni hapo Julai 3 mwaka huu kubaini kuwa wanafunzi
wawili Naftari Nganga na Collin Kisinga ndio waliochoma mabweni ya shule hiyo
huku wenzao watatu wakiwa na taarifa za mipango hiyo na hawakuripoti.
Amesema wanafunzi hao walianza mpango wa kuchoma moto mabweni mnamo
Juni 28 kwa kununua vifaa vya kuchomea, ilipofika Julai 2 walijaribu kuchoma
bweni lakini halikuwaka, Julai 3 walichoma bweni likawaka na kusababisha hasara
hiyo na Julai 6 walifanya jaribio lingine tena la kuchoma moto ghala la chakula
lakini halikuwaka moto.
Brig. Jen. Mwangela
ametoa miezi mitatu kwa wazazi wa Naftari na Collin kila mmoja alipe shilingi
milioni 7.3, Mmiliki wa Shule pia alibainika kuwa na uzembe wa kuweka vifaa vya
kuzimia moto hiyo alipie shilingi milioni 7.3 huku mwalimu wa zamu siku ya
tukio, mlinzi na Patroni nao wakitakiwa kulipa shilingi milioni 4 ili kufidia
hasara iliyotokana na ajali hiyo ya moto.
Aidha Brig. Jen
Mwangela amewaagiza maafisa elimu wote
Mkoa wa Songwe kuhakikisha wanafanya ukaguzi katika shule zote ili kubaini
endapo elimu ya tahadhari ya majanga ya moto na vifaa muhimu kwa ajili ya
kuzima moto vimewekwa katika maeneo ya shule pamoja na kuzingatia taratibu na
miongozo ya uendeshaji wa shule.
Pia amewataka
wanafunzi kuzingatia masomo na kuacha tabia za kujiingiza katika vitendo viovu
vinavyoweza kuharibu maisha yao kwani taifa linawategemea wawe wananchi bora na
viongozi au watendaji wa baadae.
Mama mzazi wa
mwanafunzi Collin aliyechoma moto shule Bi Agnes Kisinga amesema kitendo
alichofanya mwanafunzi huyo si kizuri na amesikitishwa sana huku akitoa wito
kwa walimu kushirikiana na wazazi katika malezi huku akiwaasa wanafunzi
kuzingatia masomo.
Naye Mwanafunzi Denis
Petro wa kidato cha tatu katika shule hiyo amesema tukio hilo limewasababishia
hasara kwa kuwa vifaa vya shule viliteketea kwa moto huku akiwaasa wanafunzi kuzingatia masomo na kuacha matendo
mabaya kama ya kuharibu mali za shule.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Shule ya Wavulana ya Oswe Fabian Mwalyego amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Songwe
kwa kuchukua hatua muhimu katika kukabiliana na janga la moto lililotokea shuleni hapo huku akiahidi kurekebisha
mapungufu yaliyobainika katika shule hiyo.
No comments:
Post a Comment