Na Mwandishi Wetu, Katesh
Arusha
SERIKALI ikiwa imewaonya mara
kadhaa Wakuu wa Shule za Umma, kutowachangisha Wazazi michango m inatoa Elimu
bila Malipo, Wazazi wenye kipato duni wa
Sekondari ya Balang’dalalu Katesh wamedai, wanakerwa na Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Wazazi, Nehemia Lori, anayeendelea kuwachangisha Michango
iliyokatazwa na Rais, John Magufuli, akitumia Akaunti Na. 41010012949 NMB,
Mapema Serikali ilipofunga
Shule na Vyuo kwa sababu ya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu COVIC-19, Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Lori wa Sekondari hiyo aliwataka Wazazi, kuchangia Sh. 40,000/-
na Shajala (Rim moja Rulled Paper na Plain), ambapo Wazazi wa Watoto wa Mwaka
wa kwanza waliishangaa kuchangishwa fedha hiyo, kwa maana hawajawahi kukubaliana
naye kama vipeperushi vyake vinavyoeleza.
Ujumbe wa vipeperushi vya
Machi 17, 2020, uliotumwa kwa Wazazi/Walezi Lori ulisema, “Kamati ya Wazazi
inakuomba kulipa Tsh. 40,000/- ambayo ni makubaliano ya Kikao cha Wazazi pia
rim (1) moja ya A4, na Ruled (1) moja Jina la Akaunti Kamati ya Wazazi Shue ya
Sekondari Balang’dalalu 41010012949 NMB. P.o. Box 67, Katesh.”.lilisema ombi
hilo ambalo ni mchango wa kila Mwaka.
Alipoulizwa na kuhusu malipo
hayo na Mwandishi, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Lori, alikiri ni kweli
walituma vikaratasi hivyo kwa wazazi yakiwa ni makubaliano waliyokubaliana,
ambapo Wazazi wa Mwaka wa Kwanza walikanusha hawajawahi kukaa na Kamati hiyo
wakazungumzia maombi hayo ambayo hulipwa kila mwaka (40,000/- X Wanafunzi wote
shuleni).
Alipobanwa malipo hayo ni ya
nini wakati Serikali inatoa Elimu bila malipo Lori alisema ni kwa ajili ya
kuwalipa Walimu wanaofundisha masomo kutokana na ukosefu na Uchache wa Walimu,
Walinzi, Ukarabati wa Majengo, Maji na vitu vingine ambapo wazazi walidai ni
miongoni mwa vitu vinavyowakera kama ambavyo Serikali ya awamu ya tano ya Rais,
Magufuli, vinavyomkera hasa watendaji wanapokiuka maagizo yake na
kuchomeka visingizio vyao.
Ikumbukwe; Januari 18, 2018
Rais Magufuli alisema Serikali yake inatoa Shilingi Bilioni 23.875 kila mwezi
kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa elimu bila malipo hivyo, inamshangaza kuona
bado kuna walimu wanaendelea kuwatoza michango ama kuwarudisha nyumbani
wanafunzi ambao wanashindwa kutoa michango hiyo.
“Haiwezekani! Tumefuta Ada,
halafu baadhi ya Walimu Wakuu wanaamua kuanzisha tena michango mingine mikubwa
ambayo watu maskini wanashindwa kusomesha Watoto wao”.alionya Rais Magufuli.
Katika hotuba yake ya ufunguzi
wa Bunge Magufuli alipiga marufuku michango yote ya lazima kwa wazazi katika
elimu, ambapo baada ya tamko hilo serikali ilitoa miongozo inayoelekeza namna
elimu bila malipo itavyotekelezwa kwa kuelekeza majukumu ya serikali kwa upande
mmoja na wazazi kwa upande wa pili, ingawa bado kuna wanaojiita kamati za
wazazi wanaoendeleza michango hiyo kinamna.
Miongozo hiyo ni utumiaji wa
fedha katika utekelezaji wa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari
ambao ulifafanua namna fedha ya ruzuku ya uendeshaji wa shule zitakavyotumika,
ambapo upande wa shule za msingi asilimia 30 ni kwa ajili ya vifaa vya
kufundishia na kujifunzia, asilimia 30 ukarabati, asilimia 20 gharama za
mitihani, asilimia 10 kwa ajili ya michezo na asilimia 10 ni kwa ajili ya utawala.
Awali aliposisitiza
utekelezaji wa onyo la Magufuli kuhusu tamko hilo Waziri wa Elimu Sayansi
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Ndalichako aliwataka walimu wote ambao tayari
walikuwa wamekwisha kuchangisha fedha hizo, kufanya utaratibu wa kurejesha kwa
wazazi michango hiyo na kutoendelea tena na utaratibu huo uliopigwa marufuku na
rais Magufuli.
Prof. Ndalichako aliwataka
Walimu kote nchini kufuata miongozo ya utumiaji wa fedha katika utekelezaji wa
elimu bila malipo kwa upande wa shule za msingi na sekondari kama
ulivyofafanuliwa na kuagizwa namna ambavyo fedha ya ruzuku ya uendeshaji shule
zitakavyotumika.
No comments:
Post a Comment