Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Mwanaisha Said, akizungumza na waandishi wa habari juu ya walivyojipanga kuwahudumia wananchi wanatakaofika katika banda lao lililopo kwenye viwanja wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa.
NA JANETH JOVIN
SHIRIKA la Posta Tanzania limewataka watanzania kutembelea katika banda lao lililopo kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba ili kuweza kupata huduma mbalimbali ikiwamo ya ununuaji wa stempu, utumaji barua na huduma mpya za kimtandao zilizoanzishwa na shirika hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja vya maonesho hayo, Meneja Mkuu wa Uendeshaji Biashara wa shirika hilo, Mwanaisha Said anasema wamefika katika maonesho hayo mwaka huu kwa lengo la kujitangaza, kusongeza huduma kwa wananchi na kutoa huduma mbalimbali kwa watanzania.
Anasema shirika la Posta linajiamini na lipo katika viwanja vya maonesho hayo hivyo wananchi wanakaribishwa kutembelea ili kujionea huduma zinazotolewa.
"Watanzania njooni mtuone maana sisi si wale wa zamani mliotuzoea kwani kwa sasa tunahuduma nyingi za kisasa zilizoboreshwa, kwahiyo tukasema tutumie fursa hii ya maonesho kuwaonesha watanzania tulichokuwa nacho," anasema
Anasema pia wanahuduma mpya za ubadirishaji wa fedha za kigeni aina 12, hivyo wananchi wanaohitaji huduma hiyo wasisite kufika katika maonesho hayo kubadirisha fedha zao na kuongeza kuwa wanaitangaza huduma yao mpya ya posta kiganjani.
"Tumekuja kuwaambia wananchi kuwa sasa hivi lile sanduku la barua lilikuwa linamilikiwa na ufunguo limepitwa na wakati licha ya kwamba litaendelea kuwepo, tumejipanga na kuboresha huduma kwa kutumia simu ya mkononi yaani sanduku la barua lipo katika namba ya simu ya mtu," anasema
"Kwa hiyo tumekuja kuwaambia tumehamia kidigitali, lakini huduma zetu za zamani bado zipo wasisite kuja na kuzitumia huduma zetu hapa hapa sabasaba yaani kama kuna mtu anataka kutuma barua au kununua stempu wake katika banda letu watapata huduma," anasema
Aidha anasema wanayohuduma ya duka la mtandaoni ambalo utumika kutangaza bidhaa mbalimbali za wafanyabiashara ambapo mteja ununua na kusafirishiwa bidhaa zake na shirika hilo kwa kuletewa mahali halipo.

No comments:
Post a Comment