Wakazi
wa eneo la Mvumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wamelalamikia kitendo
cha baadhi ya watu wanaohodhi mashamba makubwa kuwatoza shilingi elfu 30
ili waoneshwe mahali pa kulima mbali na kutozwa gunia moja au shilingi
laki moja kwa kila heka moja baada ya mavuno.
Hayo
yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki ambaye pia ni mjumbe Maalum katika kamati iliyoundwa
na Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kufuatilia,kutathmini na kutoa
mapendekezo na ushauri kwa Rais ili kumaliza migogoro ya ardhi ya muda
mrefu wilayani Kilosa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Mwambambale Asajile amesema
tatizo la ardhi Wilayani humo limekuwa kubwa kutokana na hulka ya
wakulima hao kuuza tena mashamba hayo pale serikali inapoyafuta na
kuyarudisha kwa wananchi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliunde
kamati maalum kwa ajili ya kutathmini na kumpa ushauri kuhusu mashamba
makubwa ambayo mengine yametelekezwa na kuwa mashamba pori ili ayafute
na kuyagawa kwa wananchi ikiwa ni jitihada za kumaliza matatizo ya ardhi
wilayani Kilosa ambayo yamekuwa yakisababisha maafa hususani baina ya
wakulima na wafugaji.
No comments:
Post a Comment