Mmoja
wa wazee katika makazi ya Msufini, akitoa burudani
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt.
John Jingu kushukuru juhudi za Serikali katika kuwahudumia wazee
wasiojiweza
nchini.
(Picha na WMJW).
Na Mwandishi Wetu, Muheza
Wazee wanaoishi kwenye makazi ya Mwanzage na Msufini Mkoani
Tanga wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kuwatunza na
kuhakikisha wanapata mahitaji yao muhimu.
Hayo yamebainishwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika makazi hayo yenye lengo
la kuona maendeleo ya uendeshaji wa vituo hivyo.
Mzee Flolian Michael amesema kuwa Serikali iliyo chini ya Rais
Magufuli imekuwa ikiwajali sana wazee wasiojiweza nchini kwa kuwekea
miumdombinu rafiki na kuwapatia huduma muhimu za malazi chakula na matibabu.
"Tunaishukuru Serikali ya Magufuli, tunapata chakula,
tunavaa, Mungu ambariki” alisema.
Naye Mzee Milton John ameomba kuangaliwa zaidi kwa kundi la
wazee wasio na walezi kwani
wamekuwa wakipatwa na matatizo mbalimbali na kukosa msaada kabisa.
“Nimshukuru Rais Magufuli kwa kutukumbuka wanyonge tusio na
waangalizi hasa sisi wazee endelee kutukumbuka wanyonge” alisisitiza
Akizungumza mara baada ya kukagua Makazi hayo Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewahakikishia
wazee hao kuwa Serikali itaendelea kuwatunza na kutatua changamoto zinazowakabili
ikiwemo kuongeza watumishi kwenye makazi yao.
"Serikali inawapenda, ina jukumu la kuwatunza ikiwemo
kuwapa matibabu, tunayo Sera ya matibabu bure kwa wazee ambayo mnaipata,
tunaelewa kuna vipimo vya ziada na hilo ni jukumu letu kugharamia" alisema.
No comments:
Post a Comment