Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro - Mathayo Masele akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la Benki ya NMB Malinyi . Wengine katika picha kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mikopo waa NMB - Demetus Kaguna, Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Salie Mlay - Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki - Dismas Prosper na Meneja wa Tawi la Malinyi - Ipyana Mwakatobe.Mkuu wa Wilaya ya Malinyi - Mathayo Masele na Kaimu Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB Salie Mlay wakipiga makofi baada ya kufunguliwa rasmi kwa tawi la Benki ya NMB Malinyi.
Na Mwandishi Wetu
Benki ya NMB imeendelea kupanua wigo wake kwa kufungua tawi ‘NMB Malinyi’ katika wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro. Ufunguzi wa tawi hili umeleta ahuweni kwa wakazi waliokuwa wanasafiri umbali wa kilomita 160 kwenda mji wa Ifakara Wilayani Kilombero kupata huduma za kibenki.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi - Mathayo Masele amesema tawi hilo limekuwa likisubiriwa kwa hamu sana kwani NMB ndio taasisi ya kwanza kufungua tawi ambapo anaamini litachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo katika eneo hilo kutokana na kuongezeka kwa kasi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo pamoja na uchimbaji wa madini ya dhahabu ambayo yamegunduliwa hivi karibuni.
Masele alisema kuwa Benki hiyo licha ya kukuza uchumi pia itawapunguzia gharama wafanyabishara, naTaasisi ambazo zilikuwa zikitumia gharama kubwa kwaajili ya kusafirisha fedha kwa usalama zaidi.
Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Salie Mlay, alisema moja ya kichocheo kikubwa cha kufungua tawi hilo ni kuwasaidia wakulima na wafugaji waweze kupata mikopo pamoja na elimu ya ushirika utakaowapa tija kwa kutumia mfuko wa NMB Foundation.
Sambamba na uzinduzi huo, NMB imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi vikiwemoa mabati, kofia,misumari na mbao kwaajili yakukamilisha uwezekaji vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Nawigo iliyopo Malinyi.
Ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.
No comments:
Post a Comment