Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma kwa wananchi walioshiriki mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika taasisi hiyo leo wakati wa mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi hundi ya Shilingi milioni 200 iliyotolewa leo katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB zilizokusanywa kutoka kwa washiriki wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi tuzo iliyotolewa leo katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB kutambua huduma zinazofanywa na taasisi hiyo wakati wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walioshiriki mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi Oyster bay leo Jijini Dar es Salaam. Picha na JKCI.
August 17, 2020
Home
Unlabelled
CRDB BENKI YACHANGIA MATIBABU YA WATOTO 100 WENYE MAGONJWA YA MOYO WANAOTIBIWA JKCI
CRDB BENKI YACHANGIA MATIBABU YA WATOTO 100 WENYE MAGONJWA YA MOYO WANAOTIBIWA JKCI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment