Viongozi wapya wa
Klabu ya Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha
ya pamoja baada ya kuchaguliwa Agosti 15/2020.
KLABU
ya Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam (DCPC), imefanikiwa kupata
viongozi wapya ambao watahudumu miaka mitatu kwa mujibu wa Katiba.
Viongozi
hao wamepatikana kupitia uchaguzi uliofanyika Agosti 15, 2020 katika
Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ilala na kusimamiwa na Wakili
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Arettas Kyara kutoka Global Advocates co.
Akizungumzia
kabla ya uchaguzi kuanzia msimamizi wa uchaguzi alitaja nafasi
zinazogombewa kuwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu
Msaidizi, Mwekahazina, Mwekahazina Msaidizi na Wajumbe Sita.
Kyara
alisema uchaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa Katiba ambapo nafasi zote
zilipata wagombea kasoro nafasi ya Mwekahazina Msaidizi.
Aliwataja
wanachama wa DCPC ambao wamejitokeza kugombea uongozi kuwa ni Irene
Mark, Angela Mang'enya na Paul Maregesi waliomba nafasi ya uenyekiti
ambapo Irene Mark alifanikiwa kushinda.
"Katika
nafasi ya Makamu Mwenyekiti waliomba ni Chalila Kibuda na John Livoti
na Chalila aliibuka mshindi. Katibu Mkuu alikuwa mgombea mmoja Hussein
Siyovelwa na amefanikiwa kushinda na Katibu Msaidizi aligombea Fatma
Jalala ambaye pia ameshinda," alisema Kyara.
Alisema
nafasi ya Mwekahazina walijitokeza watu wawili ambao ni Arodia Peter na
Patricia Kimelemeta na Kimelemeta kuibuka mshindi.
Msimamizi
huyo wa uchaguzi alisema nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambapo
walipaswa kuwa sita waliomba watu sita ambao ni Christina Gauluhanga,
Cecilia Jeremia, Shabani Matutu, Selemani Msuya, Tausi Mbowe na
Kamugisha Muchunguzi na wote walishinda hivyo kuwa wajumbe wa kamati ya
utendaji.
Kyara alisema
uchaguzi huo ulikuwa wa kidemokradia, huru na haki hivyo ni matumaini
yake kuwa viongozi waliochaguliwa watafanya kazi vizuri kujenga DCPC.
Akizungumza
baada ya uchaguzi Mwenyekiti mpya wa DCPC Irene Mark aliwaahidi
wanachama uongozi uliotukuka, kujituma, ushirikiano na ubunifu
kuhakikisha klabu inafikia malengo iliyojiwekea.
Mark
alisema DCPC inapaswa kuwa mfano wa kuigwa na klabu nyingine nchini
kutokana na wingi wa waandishi waliopo Dar es Salaam jambo ambalo
ameahidi kulisimamia.
No comments:
Post a Comment