Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa (NHIF), Angela Mziray, akizungumzia mbele wa Waandishi wa Habari Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam (DCPC) wakati wa mkutano mkuu na uchaguzi mkuu wa viongozi.Waandishi wa habari wanachama wa DCPC wakiwa katika picha ya kumbukumbu na wawakilishi kutoka NHIF baada ya kufunguliwa mkutano mkuu wa klabu hiyo mwishoni mwa wiki.
Na Suleiman Msuya
ZIADI
ya Watanzania milioni 4.4 wananufaika na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF), huku mfuko ukisisitiza wananchi kujiunga kwa wingi.
Hayo
yamesemwa na Meneja Uhusiano wa NHIF, Anjela Mziray wakati wa mkutano
mkuu na uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari jijini Dar
es Salaam (DCPC) uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Mziray
alisema NHIF ni chombo sahihi kwa usalama wa afya ya Watanzania hivyo
anawaomba waandishi kujiunga na kuhamasisha wananchi kujiunga kwa
kuandika na kuelezea faida za mfuko huo.
Alisema
Watanzania milioni 4.4 bado ni idadi ndogo hivyo wao wanaendelea kutoa
elimu kwa jamii kuhusu faida za mfuko huo kwenye maisha yao.
"Hadi
sasa zaidi ya Watanzania milioni 4.4 wananufaika na mfuko ila mikakati
yetu ni idadi hii iongezeke mara dufu hali ambayo itachochea
ustahimilivu wa mfuko.
Ila
nisisitize kuwa NHIF ni sawa na kusema msaada tutani kwani imekuwa
ikiwaokoa watu wengi wakati wanapokutwa na majanga ya kiafya," alisema
Mziray.
Kwa upande wake
Meneja Masoko na Huduma wa NHIF, Hipoliti Lelo alisema mfuko huo
umefanyiwa mabadiliko mengi ili uweze kukidhihaja za wanufaika wore
ambao wanataka kujiunga wakiwemo waandishi wa habari.
"Tuna
mifumo miwili ya kunufaika na NHIF, wapo wanaochangia asilimia 6 ambapo
mwajiri anachangia asilimia 3 na mwajiriwa 3. Ila lipo kundi
linalochangia kuanzia 50,400, 100,000 hadi zaidi ya milioni 1 wote
wananufaika na mfuko na nyie waandishi tumewapa kifurushi maalum cha
100,000 ila mmeshindwa kukichangamkia," alisema.
Lelo aliwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuandika namna mfuko huo unavyoweza kumsaidia mtu katika wakati mgumu.
Meneja
huyo aliwataka waandishi kote nchini kutumia nafasi hiyo ya upendeleo
kwa kujiunga na mfuko huo ili waweze kukabiliana na changamoto za
matibabu ambazo wanaweza kukutana nazo.
Alisema fursa hiyo ya waandishi inawahusu wenza wao hivyo wanapaswa kuitumia kikamilifu.
Akizungumzia
fursa hiyo Mwandishi Mwandamizi, Salehe Mohammed alisema watahakikisha
wanaitumia kikamilifu ili waweze kukabiliana na changamoto za matibabu.
No comments:
Post a Comment