Maganza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana wa chama hicho, alitoa ahadi hizo jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni zake ambapo pamoja na masuala mengine aliwataka wananchi hao pia kumpigia kura Mgombea wa urais kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) Rais John Magufuli.
Alisema kuwa dhamira yake endapo atachaguliwa na wananchi hao ni kuhakikisha analiletea maendeleo jimbo hilo alilodai kuwa kwa kipindi kirefu linaonekana kuwa nyuma kimandeleo chini ya uliokuwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)
Alisema kuwa endapo atafanikiwa kushinda kiti hicho, atashirikiana vyema na Serikali ya Rais John Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi hao wa Kibamba kwa madai ya kuwa anazifahamu vyema changamoto za wananchi wa eneo hilo, hatua inayompa wepesi katika kutekeleza majukumu yake” alisema Maganza ambaye kitaaluma ni mhandisi.
“Nakishukuru chama changu kwa kunituma kuja kugombea jimbo hili ambalo wananchi wake walikuwa wakiniomba nije kugombea, hii ni heshima kubwa kwangu na nina jisikia vizuri kuingia katika mchakato huu ambao utaniwezesha kuwa Mbunge hivyo kuwa karibu na Serikali katika masuala ya kimaendeleo” alisema Maganza
Alisema pamoja na chama hicho kuamua kumuunga mkono Rais John Magufuli katika nafasi ya urais, wamekubaliana kujitokeza kuwania nafasi za Ubunge na udiwani katika majimbo yote ya uchaguzi kwa lengo la kupata nafasi zitakawawezesha kwenda kumsaidia Rais katika kuliletea Taifa maendeleo.
Alisema kupitia uwakilishi wake atakwenda kulibadirisha jimbo hilo kikamilifu kwa kushirikiana na chama chake alichosema kuwa kwa dhati kimeonyesha kumuunga mkono katika uamuzi wake huo wa kwenda kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo lililokuwa chini ya Katibu wa sasa wa Chadema John Mnyika.
No comments:
Post a Comment