HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

September 19, 2020

SERIKALI ITAKAYOONGOZWA NA CHADEMA KUWEKA BIMA MAALUM YA KUWAFIDIA WAKULIMA NA WAFUGAJI WAKATI WA MAJANGA

Ili kuhakikisha wakulima na wafugaji wanakuwa salama wao na mali zao, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedhamiria kuwafuta machozi Wakulima na Wafugaji ili kupata fidia wakati wa majanga au ukame unaoathiri mazao na mifugo yao.

Ahadi hiyo imetolewa leo Jumamosi, Septemba 19, 2020 jimboni Sikonge mkoani Tabora na Mgombea nafasi ya Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalimu.

Mhe. Mwalimu amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) haina mpango wowote wa kuangalia usalama wa Wakulima, Wafugaji na Mali zao.

“Kilimo bado ni uti wa mgongo wa Tanzania kwani wananchi wengi wanajihusisha na kilimo. Lakini serikali ya CCM haijawahi kuja na mpango madhubuti wa kuwafuta machozi Watanzania pale yanapotokea majanga ya ukame, mafuriko au uharibifu unaofanywa na Wanyamapori.

“Wakulima wamekuwa hawana pa kukimbilia punde wanapopatwa na majanga. Kama watu wanaweka Bima kwenye magari na mali nyingine za ndani kwanini kusiwepo na Bima maalum kwa ajili ya mazao ya wakulima na wafugaji? Chadema tumedhamiria kuanzisha Bima kwa ajili ya wakulima wetu na wafugaji wetu,” alisema Mheshimiwa Mwalim.

Mhe. Mwalimu amesema Ilani ya Uchaguzi ya Chadema ya mwaka 2020 Sura ya 8(f) inasema Chadema imedhamiria kuweka utaratibu wa Bima kwa Wakulima na Wafugaji ili kupata fidia wakati wa majanga au ukame.

Mhe. Mgombea nafasi ya Makamu wa Rais leo alifanya mikutano kwenye majimbo ya Sikonge, Igalula na Tabora Mjini.

Kesho ataendelea na ziara kwenye mkoa huo kwa kufanya mikutano kwenye majimbo ya Tabora Kaskazini na Kaliua.
 
Mgombea Mwenza Kiti cha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo Septemba 19,2020 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui mkoani Tabora.

Mgombea Mwenza Kiti cha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Tabora Mjini, Hawa Mwaifunga, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo Septemba 19 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment

Pages