HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 20, 2020

MultiChoice yaanika mambo mazito - yaahidi makubwa kwa wateja wa DStv

Kampuni ya MultiChoice Tanzania imebainisha mambo makubwa iliyoyafanya hapa nchini tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka ishirini iliyopita ikiwemo kutoa ajira, kukuza tasnia ya filamu na Sanaa huku ikiendelea kuwa kitovu cha burudani kitaifa na kimataifa kwa wateja wake wa
DStv.


Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso wakati wa hafla maalum ya wadau wa MultiChoice.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na mmiliki wa MultiChoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe (wa pili kushoto) akiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Godfrey Mngereza (katikati), Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank, Cosmas Kimario wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yanajiri wakati wa hafla maalum ya MultiChoice Showcase iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wanahabari na wadau mbalimbali wa Sanaa na michezo, kampuni ya MultiChoice ilibainisha mikakati yake ya kuendelea kuwapatia wateja wake burudani, elimu na habari kupitia chaneli za DStv.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), mkurugenzi huyo amesema MultiChoice imekuwa kinara wa mapinduzi ya burudani hapa nchini

kwa kuhakikisha kuwa inaongeza maudhui mengi ya ndani na pia kusaidia kuimarisha tasnia ya filamu hapa nchini.
Amesema miaka mnne iliyopita, MultiChoice ilianzisha chaneli maalum ya Maisha Magic Bongo ambayo ni mahsusi kwa maudhui ya ndani. “Chaneli hii inabeba maudhui ya kitanzania kwa asilimia 98 na maudhui haya huzalishwa hapa nchini na wazalishaji na waigizaji wa hapa nchini.
Katika kipindi kifupi cha miaka minne, chaneli hii imetumia fedha nyingi kwa uzalishaji na ununuzi wa maudhui ya kitanzania na imefanya kazi na wazalishaji zaidi ya 200, waigiaji zaidi ya 2,000 na zaidi ya wasaidizi 5,000” alisema Jacqueline.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na mmiliki wa MultiChoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe (katikati mstari wa mbele), Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Godfrey Mngereza (wa pili kushoto), Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Movie wakati wa hafla maalum ya MultiChoice Showcase iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wanahabari na wadau mbalimbali wa Sanaa na michezo, kampuni ya MultiChoice ilibainisha mikakati yake ya kuendelea kuwapatia
wateja wake burudani, elimu na habari kupitia chaneli za DStv.


Katika kuimarisha tasnia ya filamu, Jacqueline amesema kuwa kampuni hiyo inashirikiana na bodi ya filamu katika kutoa mafuzo kwa wazalishaji hapa nchini ambapo mwaka 2018 walifanya
mafunzo katika mikoa mbalimbali na sasa wapo kwenye mazungumzo ya kushirikiana na bodi

ya filamu kuendesha mafunzo maalum – Master Classes kwa kushirikian na Programu ya MultiChoice Talent Factory. Programu hiyo huchukua vijana wachanga kwenye tasnia ya filamu
kutoka kote barani Afrika na kuwapatia mafunzo katika vituo maalum kwa muda wa mwaka mzima.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau mbalimbali wameipongeza kampuni ya MultiChoice Tanzania kwa jitihada zake za kutoa huduma bora na pia mchango wake katika tasnia mbalimbali hususan habari, michezo, burudani Sanaa na utamaduni.
 

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo, amesema kuwa wamekuwa na ushirikiano mkubwa wenye tija kati yao na kampuni hiyo na kwamba ushirikiano huo umezaa matunda kwa kusaidia katika kutoa ajira kwa wasanii kwa kununua kazi zao na pia kwa mafunzo mbalimbali.

Msanii nguli wa Bongo Movie Jacob Steven al-maarufu JB akizungumza kwenye utambulisho wa wasanii wa Bongo Movie wakati wa hafla maalum ya MultiChoice Showcase iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wanahabari na wadau mbalimbali wa Sanaa na michezo, kampuni ya MultiChoice ilibainisha mikakati yake ya kuendelea kuwapatia wateja wake burudani, elimu na habari kupitia chaneli za DStv.

Kwa upande wao, wasanii mbalimbali wa Bongo Movie hapa nchini wamesema kuwa MultiChoice kupitia DStv imekuwa mkombozi mkubwa kwao kwani wamekuwa wakichukua kazi
nyingi za wasanii wa ndani na hivyo kuwawezesha kiuchumi na kitaaluma pia.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na mmiliki wa MultiChoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe (katikati) akiwapongeza watangazaji maarufu Salama Jabir (kushoto) na Abuubakar Lyongo ambaoni miongoni mwa watangazaji wanaotangazi ligi kuu ya soka ya Uingereza kwa lugha ya Kiswahili kupitia SuperSport wakati wa
hafla maalum ya MultiChoice Showcase iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wanahabari na wadau mbalimbali wa Sanaa na michezo, kampuni ya MultiChoice ilibainisha mikakati yake ya kuendelea kuwapatia wateja wake burudani, elimu na habari kupitia chaneli za DStv.


Wadau wengine wakiwemo waandishi wa habari, wamesema kuwa MultiChoice imesaidia sana katika kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia hususan kwenye upande wa michezo. Wakizungumza katika hafla hiyo, watangazaji maarufu wa michezo nchini Abuubakar Lyongo, Maulid Kitenge, Oscar Oscar na wengineo ambao ni miongoni mwa watangazaji wa ligi kuu ya soka ya Uingereza kwa lugha ya kiswahili, wamesema kuwa kuoneshwa kwa mashindano ya
kimataifa kunawafanya watanzania kujifunza mengi na hivyo kuongeza ushindani.

No comments:

Post a Comment

Pages