HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 20, 2020

Wateja 240 wa Benki ya CRDB kuzawadiwa kila siku

Mkuu wa Kitengo cha Masoko Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jipe Tano" inayolenga kuhamasisha wateja kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. Benki ya CRDB imetenga Shilingi milioni 100 kama zawadi kwa wateja ambao watakuwa wakiweka akiba mara kwa mara katika akaunti zao, ambapo wateja 240 watakuwa wakijishindia fedha kila siku.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Benki ya CRDB, Stephen Adili akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jipe Tano" inayolenga kuhamasisha wateja kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. Benki ya CRDB imetenga Shilingi milioni 100 kama zawadi kwa wateja ambao watakuwa wakiweka akiba mara kwa mara katika akaunti zao, ambapo wateja 240 watakuwa wakijishindia fedha kila siku.


Na Irene Mark


BENKI ya CRDB imezindua kampeni ya kuwazawadia wateja wake wanaojiwekea akiba ambapo kila siku wateja 240 watapata zawadi hizo baada ya kuweka akiba kwenye akaunti zao.
 
Kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi Oktoba 16 mwaka huu na itaendelea hadi Desemba 31 ambapo wateja wakaoweka akiba zao kwa njia mbalimbali watapewa zawadi ya sh.5,000 zitakazoingozwa kwenye akaunti zao.

Akizungumza na wanahabari mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda, alisema zawadi hizo zitatolewa kwa wateja wa akaunti zote.

“Leo tunazindua kampeni yetu ya ‘Jipe Tano’ hii ni katika kuhamasisha wateja wa benki yetu ya CRDB kujiwekea akiba lakini pia tunaelekea kipindi cha sikukuu na Januari.

“Tunapoanza mwaka tunakumbana na ada za shule, kodi za nyumba na mambo mengine mengi ndio maana wanauita ‘Njaanuari’ wakimaanisha ni mwezi mgumu kifedha... sisi tunataka kumsaidia mteja wetu kuianza Januari bila msongo wa mawazo,” alisema Kamuhanda.

Alisema Benki ya CRDB itatoa sh. milioni 1.2 kila siku kwa wateja wake watakaoweka akiba kwenye akaunti zao kwa njia ya simu za mkononi, mawakala, kupitia atm mashine au ndani ya tawi la benki hiyo watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujishindia sh. 5,000 kila wanapoweka.

“Watanzania wote, tumehakikishia kwamba tumeweka vigezo rafiki sana ili watu wengi waweze kushiriki na kushinda. Ili kuweza kushiriki na kupata nafasi ya kujishindia zawadi utatakiwa kuwa na akaunti hai ya Benki ya CRDB,” alisisitiza Kamuhanda.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi cha Benki ya CRDB, Stephen Adili, alisema mteja atakayeweka kuanzia sh. 50,000 kwenye akaunti yake anajihakikishia ushindi wa ‘Jipe tano’.
 
Alisema kampeni hiyo itawahusu wateja wenye akaunti mbalimbali katika benki ya CRDB zikiwemo akaunti za watoto, wanawake, wanafunzi na nyinginezo.

“Mteja anaweza kuweka akiba yake kwa kwenda kwenye moja kati ya matawi zaidi ya 240 ya benki ya CRDB, kwa CRDB Wakaka, kupitia simbanking, internet banking na njia zote za mteja kuifikia akaunti yake.

“...Pia wateja watapata ushauri ushauri wa uhifadhi wa fedha kutoka kwa wataalamu wa fedha waliopo katika matawi yetu. Kwa mfano tu, wakina mama watapata ushauri mahususi kutoka kwa mtaalamu aitwae ‘Malkia Rafiki’ juu ya kutunza fedha kupitia akaunti yake ya Malkia. 

“Hivyo hivyo kwa wastaafu kwa ajili ya utunzaji wa Pensheni zao na walezi wanaopanga kuweka akiba kwa ajili ya watoto. Tunawakaribisha sana wote,” alisema Adili.

No comments:

Post a Comment

Pages