Na Irene Mark
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Jenga Afya, Tokomeza Umaskini (JATU), Dk. Zaipuna Yona ameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi yaliyoifanya kampuni hiyo kuingia kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa wanahisa, wanachama na marafiki wa JATU, Dk. Yona alisema hizo ni hatua bora za ukuaji wa uchumi wa kampuni na watanzania wote.
“Kuingia DSE kuanzia Novemba 23 mwaka huu ni moja ya malengo ya uwepo wa JATU sisi tulianza mwishoni mwishoni mwa mwaka 2016 utaona sasa tunavyokua kwa kasi leo miaka minne tayari lengo letu kubwa tumelifikia.
“Na hii sio kwa nguvu zetu bali mazingira bora yaliyoifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati yametubeba ndio maana JATU tunaishukuru sana serikali ya awamu ya tano,” alisema Dk. Yona.
Alifafanua kwamba hivi sasa watanzania wote wanapata fursa ya kuwa wanahisa wa JATU ambapo hisa moja itauzwa kwa sh.240 huku akibainisha kwamba hivi sasa kampuni hiyo itakuwa ya kimataifa.
Meneja wa JATU Saccos, Esther Kiuya alisema ni wakati wa watanzania kuanza kufaidi matunda ya kampuni ya JATU popote walipo duniani.
“Hii ya sisi JATU kuingia kwenye soko la hisa itaongeza wigo wa wawekezaji duniani kote kuifahamu kampuni yetu ambayo kwa asilimia zote inamilikiwa na watanzania,” alisema Kiuya.
Kampuni ya Jatu inajishughulisha na kulima mazao ya chakula, kuyaongezea thamani, kutafuta wateja kwa njia ya mtandao na kuwapa faida walaji wa mazao hayo.
November 15, 2020
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment