Wadau wa uhifadhi wa misitu na
mazingita wakiwemo Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili
Tanzania(TFCG)
Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA), maofisa wa
idara mbalimbali za mazingira kutoka serikalini pamoja na maofisa wa
ubalozi wa Uswisi wakiwa katika kikao cha utambulisho baada ya kufika
ofisini kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Idara ya Ajira na Kipato kutoka Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania Peter Sidler(kulia)akiwa na maofisa wengine wakijadiliana jambo kabla ya kuingia katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Iringa.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Elia Luvanda akizungumza mbele ya wadau wa uhifadhi wa misitu na mazingira. Aliyekaa ni Mkurugenzi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG) Charles Meshack.
NA SULEIMAN MSUYA, IRINGA
NCHI
ya Uswisi imesema inaridhishwa na mafanikio ya Miradi ya Usimamizi
Shirikishi wa Misitu ya Jamii Tanzania (USMJ) ambayo inatekelezwa
nchini.
Miradi ya USMJ
inatekelezwa chini ya Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa
Tanzania (TTCS) na Mradi wa Kuhifadhi Misitu kwa Kuwezesha Biashara
Endelevu ya Misitu (CoFoREST) chini ya ufadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Uswisi (SDC) na kuratibiwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu
Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania
(MJUMITA) na Shirika la Kuendeleza Nishati Tanzania (TaTEDO).
Akizungumza
katika ziara ya wajumbe wa kamati ya ushauri ya mradi iliyotembelea
Kijiji cha Mahenge kilichopo Kata ya Mahenge, Tarafa ya Mahenge wilayani
Kilolo mkoani Iringa, Mkuu wa Idara ya Ajira na Kipato kutoka Ubalozi
wa Uswisi, Peter Sidler amesema ameridhishwa na miradi ambayo
wanafadhili jambo ambalo linawapa nguvu kuendelea kufadhili.
Sidler
amesema ushirikiano wa Tanzania na Uswisi una zaidi ya miaka 30 hivyo
matarajio yao ni kuendeleza hasa kwa kugusa kundi kubwa la jamii
vijijini.
Mwakilishi huyo
amesema takwimu zinaonesha Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza kwa
uharibifu wa misitu hivyo miradi ya USMJ inayotekelezwa inapaswa kuungwa
mkono ili kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema
shughuli za uhifadhi zinazofanyika Kijiji cha Mahenge zimeonesha picha
nzuri kuwa jamii ipo tayari kutunza na kuhufadhi misitu yao na kunufaika
hivyo wataendelea kuwezesha taasisi kama TFCG na MJUMITA ili kuendeleza
malengo ya wanavijiji.
Mkuu
huyo wa idara amesema misitu ikitumiwa kwa dhana shirikishi itachochea
mabadiliko makubwa ya kiuhifadhi, kiuchumi, kijamii na maendeleo.
"Sisi
kama Ubalozi wa Uswisi tunaridhishwa na hali ya USMJ inayotekelezwa kwa
vijiji vya mradi jambo ambalo linatupa nguvu kuendelea kufadhili kwani
ni njio muhimu ya kupunguza umaskini na kuongeza uhifadhi," amesema.
Sidler
amesema wao kama ubalozi wanasaidia sehemu kidogo ya uhifadhi na
kuboresha maisha ya wananchi lakini jukumu kubwa lipo chini ya Serikali
na wananchi wenyewe.
Amesema
ni vema wadau wote wakashiriki katika uhifadhi ili kuweza kukabiliana
na athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yana madhara makubwa
duniani kwa sasa.
Mkuu
huyo wa idara amesema mwitikio wa wananchi katika USMJ ni mkubwa hivyo
ni jukumu la viongozi kushirikiana nao ili kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi.
Aidha,
amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
kuhakikisha sekta zote zinahusika katika kuondoa umaskini.
Amesema Tanzania imejaliwa misitu mingi ambayo ikitunzwa vizuri itaweza kuchochea uwepo wa hali ya hewa nzuri.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa TFCG, Charles Meshack amesema Tanzania ina
hekta milioni 48.8 za misitu ambapo hekta milioni 22 ipo katika ardhi za
vijiji ambapo hekta milioni 5 ndio ipo kwenye USMJ huku hekta milioni
17 zikiwa hazipo kwenye usimamizi.
Amesema
TFCG na MJUMITA wameamua kuja na mradi wa TTCS NA CoFoREST ili
kuwezesha wananchi kutambua umuhimu wa utunzaji wa misitu.
Meshack
amesema iwapo hakutakuwa na jitihada za kuhifadhi misitu ni wazi kuwa
ndani ya miaka 40 ijayo misitu itatoweka kwani kwa sasa kila mwaka hekta
469,000 zinapotea.
"Miradi
hii ambayo tunawapelekea wananchi ina malengo makuu matatu ambayo ni
kuhamasisha wananchi kuhifadhi misitu ya asili na kuvuna kwa uendelevu
na wanapovuna kwa undelevu kipato wawekeze kwa shughuli za wananchi na
uhifadhi.
Kusaidia
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili nchi isiwe jangwa. Lengo
kubwa ni kuwapa wanavijiji motisha wananchi wasigeuze misitu mashamba
badala yake waweze kuvuna kwa uendelevu mkaa na mbao," amesema.
Mkurugenzi
huyo amesema miradi ya USMJ ambayo wameibua kwa taktibani miaka saba
sasa imeweza kuchochea maendeleo, kukuza uchumi na kuchochea uhifadhi.
Meshack
amesema katika vijiji zaidi ya 30 ambvyo vinatekeleza mradi vimeweza
kuboresha sekta ya elimu, afya, maji, kilimo na mikopo ambapo wanavijiji
wamekusanya zaidi shilingi bilioni 3.
"Tumewekeza takribani bilioni 12 kwa awamu ya kwanza na pili lakini pia zaidi ya sh.bilioni 3 zimepatikana," amesema.
Amesema
awamu hii ya tatu wanatarajia kuwekeza shilingi bilioni 7 kwa kipindi
cha miaka mitatu ambapo wanajikita kujengea uwezo wataalam ili ziweze
kutekeleza zenyewe.
Mkurugenzi
huyo amesema kupitia miradi hiyo wamefanikiwa kurasimisha ardhi za
vijiji kuwa za kisheria jambo ambalo linatoa uhakika wa kupangia kazi
kisheria.
Amesema
Serikali inapaswa kutoa kipambele katika sekta ya mazingira na misitu
ili iweze kuwa endelevu na kuondoa sheria vikwazo katika kusimamia
misitu akitolea mfano GN417.
Mkurugenzi
wa MJUMITA, Rahima Njaidi amesema TFCG na MJUMITA zimedhamiria kuleta
mabadiliko chanya kwenye sekta ya misitu na mazingira nchini
Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Elia Luvanda amepongeza nchi ya
Uswisi, TFCG, MJUMITA na wadau wengine wanapigania USMJ kwani ni muhimu
kwa maendeleo nchini.
Luvanda
amesema Mkoa wa Iringa utashirikiana na wadau wote ambao wamedhamiria
kuhifadhi na kutunza misitu kwa kuwa ni muhimu kwa maendeleo, uchumi,
kisiasa na kijamii.
Ofisa
Maliasili wa Mkoa wa Morogoro, Joseph Chuwa amewataka wanakijiji wa
Mahenge kutumia fursa ya mradi huo kufanya mabadiliko chanya kijijini
hapo.
"Mimi nipo Morogoro
natambua faida za hii miradi nawaomba msirudi nyuma kwani ina faida ya
kiuchumi, kijamii, maendeleo na uhifadhi," amesema.
Mtafiti
Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti Tanzania (TAFORI), Dk.Charlestino
Balama amewashauri wataalam na wananchi kutafuta watafiti ili kuweza
kubaini fursa zote zilizopo katika misitu wa Mahenge.
"Watafiti
tunapaswa kuja huku kwenye Msitu wa Mahenge kwani kuna fursa nyingi
nimeziona hapa kama kuwepo vipepeo, ufugaji nyuki, madini na vingine
vingi," amesema.
Akizungumzia
mradi huo Mtaribu wa Mradi wa CoFoREST Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
Aigen Mwilafi amesema mradi huo umewezesha uandaaji wa mipango ya USMJ
na mipango ya matumizi bora ya ardhi.
Aidha
ametoa ombi kwa TFCG pamoja na wadau wake waendelee kuiwezesha
halmashauri hiyo katika suala la uhifadhi wa misitu ya vijiji kwa
kuitenga na kuhuwisha mipango ya usimamizi shirikishi ya vijiji
iliyopitwana wakati.
Aidha
amesema kuna takribani misitu 11 haijatengwa kuwa misitu ya hifadhi ya
vijiji na kuna mipango ya usimamizi shirikishi wa misitu ya vijiji 45
imepitwa na wakati inahitaji kuhuhishwa.
Hivyo
wangependa misitu yote katika vijiji vyao itengwe na kuwa misitu ya
hifadhi ya vijiji na iwe na mipango iliyohuwishwa na kupitishwa katika
ngazi zote za kisheria.
"Tunaomba muendelee kushirkiana nasi katika kutekeleza hayo," amesema.
Ametumia
nafasi hiyo kueleza TFCG imekuwa ikifanya kazi za uhifadhi kwa
kushirikiana na halmashauri ya Wilaya ya Kololo tangu mwaka 2007 na
kwamba TFCG na MJUMITA kwa kushirikiana na halmashauri iliunda mtandao
mitandao ya jamii ya usimamizi wa misitu ya asili minne.
Ameongeza
na kuanzisha mpango wa uvunaji wa mazao wa mazao ya misitu wa
Wilaya.Pia kuanzisha mitandao mingine mipya katika kata za Mahenge na
Nyanzwa na kwamba mwanzoni mwa Machi 2020 timu ya watalaam wa mradi kwa
kushirikiana na halmashauri walitembelea vijiji vya Ikula, Mahenge,
Mgowelo na Udekwa kwa lengo la kutembelea misitu na kuona kama inakidhi
vigezo vya kutekelezwa mradi wa mkaa endelevu na kuzungumza na viongozi
wa vijiji husika.
"TFCG
na wadau wake kupitia mradi huu ,mpaka sasa imeweza kuwajengea uwezo
watalaam 17 kutoka ngazi ya halmashauri na wanne kutoka ngazi ya kata
kwa kutoa mafunzo mbalimbali. Kijiji cha Mahenge ambacho ndicho
kinatekeleza mradi huu kumefanyika mikutano ya vitongoji kwa ajili ya
kuutambulisha mradi.
"Pia
kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi, mipango ya usimamizi
shirikishi wa misitu ya kijiji na kupitishwa na mkutano mkuu wa
kijiji.Kuna mafunzo yanaendelea ya uzalishaji mkaa endelevu na
uzalishaji wa mbao,kwa wazalishaji mkaa na wapasuaji mbao ambao walikuwa
wanajishughulisha na shughuli hizo hapa kijijini bila kufuata
taratibu,"amesema Mwalifi.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo Said Mhina amesema wameomba
msaada wa kupatiwa mafunzo zaidi ambapo amefafanua licha ya kuelimishwa
bado wanaomba waendelee kupatiwa elimu zaidi na kwamba wanamini kile
ambacho kitapatikana kitasaidia kuleta maendeleo ya kijiji chao.
No comments:
Post a Comment