NA MWANDISHI WETU
WAANDISHI wa habari na vijana wanaofanya tafiti katika masuala ya uchumi, elimu, biashara na Masoko wametakiwa kujikita katika kuandika makala mbalimbali zitakazolenga kuleta mapinduzi katika sekta hizo.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la COMALISO la nchini Zimbabwe Rejoice Ngwenga wakati wa semina ya simu moja kwa waandishi wa habari na vijana watafiti iliyoandaliwa na Taasisi inayojihusisha na masuala ya elimu, utetezi na Masoko ya Liberty Sparks.
Ngwenga amesema uandishi wa makala ni kipaji kama vilivyo vipaji vingine hivyo vijana wasisite kuvionyesha kwa kuandika makala ambazo zitalenga kunisaidia jamii.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Liberty Sparks, Evans Exaud amesema ni.muhimu pia vijana wanatambua masuala ya soko huria na kujenga jamii iliyohuru na yenye maendeleo.
"Waandishi tumieni maarifa mtakayopatiwa katika semina hii kuleta mabadiliko katika uchumi kwa kuandika zaidi makala zinazohusu uchumi, elimu, biashara na Masoko," amesema.
No comments:
Post a Comment