HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 11, 2021

Maalim Seif afungua kituo cha kukeshea na kumkafini maiti

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka Mashekhe nchini kuwashirikisha na kuwafundisha vijana katika masuala ya kumuaandaa maiti hadi kuzikwa kwake ili kuendeleza utaratibu huo katika jamii.

 

Alisema kuwa wakifundishwa vijana utamaduni huo wa dini ya  Kislamu utasaidia sana kwani wazee wakiwa hawapo vijana wanaweza kufanyakazi hiyo.

 

Maalim Seif aliyaeleza hayo jana huko Masjid Barza Mji mkongwe wakati akifungua kituo cha kukoshea na kumkafini Maiti kilichojengwa na msaada ya wazanzibar wanaoishi nje ya chini kupitia Jumuiya yao ya Tears Joy.

 

“Hivi ssa kila mkosha maiti utamuona ni mtu mzima vijana wakiwa pembeni sasa hili tuliondosheni” alisema Maalim Seif.

 

Aliwasihi Mashekhe hao kuelekeza juhudi zao yingi kwa vijana kwa sababu watu wanakufa kila siku.

 

Madrasa zetu zina mchango mkubwa katika malezi na makuzi kwa maisha ya vijana hapa  dunia na akhera”.

 

Makamu wa kwanza alieleza kuwa kwa sababu waalimu wa Madrasa hutumia nguvu na nafasi kubwa katika kuwafundisha vijana na Serikali kwa nafasi yake inaandaa mpango nzuri dhidi ya waalimu hao.

 

“Hatuwezi kufanikiwa katika dunia hii kama elimu ya dini tutaipa mgongoo” alisema

 

Aliwafahamisha Mashekhe hao kuwa wengine wawalee ili waweze kuvaa viatu vyao vya uongozi.

 

Sambamba na hilo Maalim Seif aliwashukuru sana wazanzibar  hao kwa mchango huo na kwaeleza kuwa wamefanya jukumu lao la kuondoa shida kwa jamaa zao.

 

“Kituo hichi walichokijenga kitaisaidia sana kwa watu wa mji mkongwe na kwa yeyote yule anayetaka kutayarishiwa maiti wake, kwani hii si kwa watu mji mkongwe ni kwa waislamu woote” alieleza.

Alisema fikra ambayo ilizaliwa na Tears Of Joy ni nzuri na kuwataka mitaa mengine kuiga jambo hilo hasa mjini kuondoa kikwazo cha kumkosha maiti.

 

Mapema akizungumza mwakilishi wa Jumuiya hiyo ya wazanzibar wanaoishi nje Suleiman Ahmed Sadikk alisema jumuiya yao iiaza na watu kumi katika nchi Uingereza lakini iko dunia nzima na iliaza mwaka 2019.

 

Alisema lengo kuu la kuunda jumuiya ni kuona wanapata nafasi ya kusadia nchi yao ili kuondoa baadhi ya kero zinazowakabili

 

Alisema katika kituo hicho wametuma milioni 26 za kitanzania mpaka kukamilika kwake.

 

“Tulipoletewa wazo hili la kujenga kituo cha kukoshea na kukafini maiti tulikaa na tukaona ni jambo jema mnoo kwa hapa duniani na kesho akhera” alisema Sadikk.

 

Alisema kuwa wamejenga kituo hicho kwa ajili ya waislamu wa aina zoote hata wale wanaotaka kusafirisha maiti zao kwa boti.

 

Akimkaribsha  makamu wa Kwanza Profesa Hemed Hikman Rashid Mwenyekiti wa Bodi ya Alnour Islam Center alisema Uislamu unamuheshimu sana binaadamu tangu kuzaliwa hadi kufa kwake.

 

Alisema kituo hicho kittumika bure na hakutakuwa na malipo yoyote kwa nayetaka kuayarishiwa maiti.

No comments:

Post a Comment

Pages