HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 31, 2021

MKUU WA MKOA WA PWANI KUKOMESHA VITENDO VYA WAHAMIAJI HARAMU WANAOINGIA KUPITIA BANDARI BUBU


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi  Evarist Ndikilo.

 

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI 

 

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amelitaka jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kuhakikisha kwamba  linaweka mikakati madhubuti kwa ajili ya kuthibiti wimbi la uaharifu pamoja na kukomoshe kabisa  matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo bangi pamoja na unywaji wa pombe halamu ya gongo ambayo inamadhara makubwa kwa afya ya binadamu.

 

Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na  askari wa jeshi la polsi kutoka wilaya mbali mbali za Mkoa wa Pwani wakati wa sherehe maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuuaga mwaka wa 2020 na kuukaribisha mwak mpya wa 2020 pamoja na  kuweza kupanga mikakati ya kulinda hali ya ulinzi na amani pamoja na kujadili changamoto zilizopo kwa skari polisi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Ndikilo alisema kuwa kumekuwepo kwa baadhi ya maeneo bado kuna baadhi ya watu wanajichukulia sheria mikononi na kusababisha kupelekea uvinjifu wa amani hivyo namuagiza Kamnada wa polisi Mkoa wa Pwani kuhakikisha kwamba analilisimaia suala hili kikamilifu na kuongeza zaidi doria katika maeneo mbali mbali lengo ikiwa ni kuimarisha hali ya ulinzia kwa wananchi.

 

“Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani nashukuru sana kupata mwaliko katika sehehe hizi ambazo zimeandaliwa na jeshi la polisi lakinikitu kikubwa ninachowaomba ni lazima sasa kuweka mipango mizuri ya kutekeleza wajibu wetu ipasavyo maana katia baadhi ya maeneo bado kuna watu wanaendelea kufanya vitendo vya uharifu hivyo ni lazima kuwabaini wale wote ambao wanahatarisha uvunjifu wa amani na wakamatwe na wachuliwe hatua kali za kisheria,”alisema Ndikilo.

 

Aidha NNdikilo alibainisha kwamba anachukizwa sana kuona bado kuna baaadhi ya wananchi wananedelea kutumia pombe aiha ya kongo amabyo ni halamu hivyo ameliagiza jeshi hilo kufanya msako mkali kwa ajili ya kuwakamata wale wote ambao watakutwa wanatumia pombe hiyo na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Kadhalika alisema serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaweka misingi imara katika kulinda nchi yake katika sehemu mbali mbali hivyo askari wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine mbali mbali vya dola wakaendelea kufanya doria za mara kwa mara katika mipaka ili kuthibiti waharifu na watu wengine wasiingie nchini kinymemela na kuja kufanya uharifu.

 

“Kumekuwepo na wimbi la wahamiaji haramu ambao wanaingia nchini kinyemela pasipo kuzingatia sheria nataratibu hivyo naliagiza jedhi la polisi pamoja na maafisa mbali mbali wa ulinzi kuhakikisha  wanalinda mipaka ya nchi ya sehemu nyingine ambazo baadhi ya raia wa kigeni wanatumia njia hizo katika kupita na kuingia nchini hasa katika maeneo ya bandari bubu kama vile maneo ya Wilayani Bagamoyo,”aliongeza Ndikilo.

Pia katika hatua nyingineMkuu huyo wa Mkoa alilipongeza jeshi la polisi Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuweka miakati ya kupunguza ajali mbali mbali za barabarani kwa kiwango kikubwa na kuwataka watumiaji wa vyombo  vya usafiri kuhakikisha kwmaba wanazingatia sheria zote za barabarani ili kuepikana na ajali amabzo zinapelekea watu kupoteza maisha yao na wengine kupata ulemavu.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa alimuahidi Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani kuzishugulikia changamoto mbali mbali zilizopo na kwamba ataendelea zaidi kulivalia njuga suala la wimbi la uharifu kwa lengo la kudumisha hali ya ulinzia na usalama.

No comments:

Post a Comment

Pages