Mwenyekiti wa Kundi la Simba Jamii Tanzania Enterprises (SJTE), aliyemaliza muda wake, Gabriel Ntole akizungumza na wanachama wa Kundi hilo pichani hawapo, kushoto ni Mlezi wa SJTE, Hassan Mbilili na Kulia ni Mjumbe kwa Kamati Tendaji James Tindi.
NA SULEIMAN MSUYA
WANACHAMA
wa Kundi la Simba Jamii Tanzania Enterprises (SJTE), wametakiwa
kushikamana na kushirikiana ili kuhakikisha kundi hilo linadumu na kuwa
endelevu.
Rai hiyo
imetolewa na Mwenyekiti SJTE aliyemaliza muda wake, Gabriel Ntole wakati
akizungumza kwenye mkutano mkuu na uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar
es Salaam.
Ntole amesema
makundi au taasisi mbalimbali zinazohuisisha jamii yamekuwa yakifunjika
kutokana na kukosekana kwa mshikamano na ushirikiano baina ya wana
kikundi.
Amesema msingi wa mshikamano na ushirikiano unaweza kufanikiwa iwapo viongozi watakuwa wavumilivu na kutunza ndimi zao.
"Kundi
hili ni kubwa na linafahamila kila mahali Serikalini hivyo wapo kati
yetu wanaona wivu na wengine wametoka hali ambayo inachangia majungu
yasiyo na sababu.
Rai yangu ni nyie viongozi kujiepusha na majungu hayo ili kuijenga SJTE yenye nguvu na mafanikio tele," amesema.
Mwenyekiti
amesema kila mwanachama anapaswa kuipigania SJTE kwa nguvu zote ili
iendelee kuwa taasisi kubwa na yenye tija kwa nchi.
Aidha,
Ntole amewataka wana SJTE kuhakikisha wanafanya uchaguzi wa viongozi
kwa kuzingatia sifa ambazo zitawasaidia kuipeleka mbele na sio
kuendekeza majungu.
Kwa
upande wake Mlezi wa SJTE, Hassan Mbilili aliwataka wana kikundi kuacha
kutumia muda mwingi kuendekeza majungu kwani hayana faida na kundi.
Mbilili amewashauri wana SJTE kutumia kundi hilo kutafuta fursa mbalimbali na sio kuendekeza umbea ambao hauna faida.
"Mimi
ni moja ya waanzilishi wa kundi hili tumepitia mengi ila hatujakata
tamaa naomba viongozi wapya mjipange na kukabiliana na changamoto zote
zitakazokuja," amesema
No comments:
Post a Comment