HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 03, 2021

MAALIM SEIF AWATAKA WAZANZIBAR KUDUMISHA UMOJA WAO

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wazanzibar kudumisha utamaduni wao ili kuendeleza umoja wao ambao utaongeza mapenzi miongoni mwao.

 

Alisema wazanzibar wamebahatika kuzungumza lugha moja  ya kiswahili ambayo inaunganisha vijiji mbali mbali hivyo iwe ni kigezo kikuu cha    kuwaunganisha wazanzibar pale panapotokea migogoro miongoni mwao.

 

 

Maalim  Seif aliyaeleza  hayo Micheweni katika ukumbi wa shule ya sekondari Karume wakati akizungumza na wananchi kupitia  makundi maalumu ikiwemo wavuvi, wakulima wa Mwani, Wajane, waendesha Bodaboda, wajasiriamali pamoja wanafanyabiashara na wenye Mahitaji maalumu na Vijana  na Viongozi wa serikali ya Wilaya ya Micheweni Mkoa Kaskazini Pemba.

 

Alisema kuwa lugha ya Kiswahili imekuwa chombo kizuri sana cha kuwaunganisha wazanzibar kwa kile alichokieleza hakihitaji mkaalimani miongoni mwao.

 

“Kuna nchi za wenzetu zinapatashida kuwasiliana kutokana kila kabila wanalugha zao hapo lazima watafute lugha nyengine ya kuwasiliana, lakini sisi Alhamdulillah lugha yetu ni moja tu ya Kiswahili ” alisema Makamu wa Kwanza wa Rais huyo.

 

Alisema ukimchukuwa mtu wa Pemba na Unguja wote huwezi kuwabaguwa anakotokea na kuhoji kwa nini watu wagombane.

 

Aliwataka wananchi hao wa Wilaya ya Micheweni kutumia utamaduni huo aliuoueleza kuwa ni kama Zawadi iliyotaka kwa muumba wao.

 

Aidha  maalim Seif aliwambi wananchi hao kwamba kila mmoja afuate dini yake  kwa kurudisha umoja na upendo kwani vyama ni mambo ya kupita, huku wakitambuwa kuwa viongozi waliopo madarakani ni viongozi wa wananchi wote na sio chama fulani.

 

“Kila mmoja atakwenda kuulizwa alifanya nini kuondoa chuki na migogoro miongoni mwa wazanzibar, lazima turudi kwa mola wetu kwani tumemkosea” alisema Maalim Seif.

 

Mapema  Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba  Salama Mbarouk Khatib alisema mkoa huo uko katika hali ya amani na utulivu na wananchi wake wote wanaunga mkono maridhiano yaliyopo.

 

Kwa upande wao wananchi hao walimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa wao hawana mashaka na maridhiano hayo lakini ni vyema hali zao za zikaandaliwa ili kuondoa mashaka miongoni mwao.

 

Sharifu Kombo Said alisema yeye alipoteza mwanae katika uchaguzi huu uliopita na kwa sasa inapotajiwa uchaguzi roho ziko juu.

 

“Kama tumetaka Maridhiano ni vyema yakatoka moyoni na kumuogopa muumba wetu ili tuondoe matatizo ambayo hutokea  kila kipindi cha Uchaguzi” alisema Said.

 

Kiongozi wa Dini ya Kiislamu wilaya hiyo Sheikh Omar Khamis alisema umoja ni kitu ambacho kimepewa uzito mkubwa katika dini hiyo.

 

Aliwataka viongozi wananchi kwa ujumla kuwa kitu kimoja katika kuiisimami na kuiongoza Zanzibar.

 

“Hatuna mbadala wa Zanzibar Vyama vya Siasa vitapita lakini Zanzibar yetu ipo”

 

Fatuma Mwinyi ambaye ni mjane alisema wajane hawanakazi kwa hiyo ni vyema Serikali ikashusha bei ya Vyakula ili na wao waweze kuzimudu.

 

Sisi ni wajane kipesa tunachokipata ni kidogo kwa lakini kama bei za vyakula zitapunguwa itakuwa bora

 

Makamu wa Kwanza wa Rais yuko kisiwani Pemba kuzungumza na wananchi kuonyesha umuhimu wa uwepo wa maridhiano katika kuendesha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

Pages