Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyango, akitoa maagizo ya kukamatwa kwa msimamizi wa Bandari ya Katembe Magarini, Maduhu Makajanga.
Na Lydia Lugakila, Muleba
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, Mhandisi Richard Ruyango, ameagiza kukamatwa kwa msimamizi wa bandari ya Katembe Magarini, Maduhu Makajanga, kutokana na tuhuma ya kuwatoza tozo kubwa ya ushuru wafanyabiashara wa samaki kinyume na utaratibu wa Serikali baada ya wafanyabiashara hao kulalamikia kitendo hicho.
Hayo yamejiri baada ya mkuu wa wilaya huyo kutembelea bandari hiyo na kuzungumza na wafanyabiashara hao katika mwaro huo.
Wakilalamikia Hali hiyo wamesema kuwa awali walikuwa watozwa ushuru wa Kawaida unaoendana na maelekezo ya Serikali licha ya bandari hiyo kuanza kupadisha tozo hivyo na kuwalazimu kutumia badari Nyingine ya Mngaza iliyopo Wilayani chato.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango baada ya kusikiliza malalamiko hayo ameamuru msimamizi huyo wa bandari akamatwe ili ahojiwe na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU).
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Mhandisi Richard Ruyango ameagiza kukamatwa kwa msimamizi wa bandari ya Katembe Magarini Bwana Maduhu Makajanga kutokana na tuhuma ya kuwatoza tozo kubwa ya ushuru wafanyabiashara wa samaki kinyume na utaratibu wa Serikali hii ni baada ya wafanyabiashara hao kulalamikia kitendo hicho.
Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango kutembelea bandari hiyo na kuzungumza na wafanyabiashara hao katika mwaro huo.
Wakilalamikia Hali hiyo wamesema kuwa awali walikuwa watozwa ushuru wa Kawaida unaoendana na maelekezo ya Serikali licha ya bandari hiyo kuanza kupadisha tozo hivyo na kuwalazimu kutumia badari Nyingine ya Mngaza iliyopo Wilayani chato.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango baada ya kusikiliza malalamiko hayo ameamuru msimamizi huyo wa bandari akamatwe ili ahojiwe na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa. (TAKUKURU).
No comments:
Post a Comment