Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) imemtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa nchi hiyo baada ya kupata kura 5,852,037 sawa na asilimia 58.64 ya kura zote zilizopigwa.
Naye mpinzani mkubwa wa Museveni ambaye pia ni mwanamuziki Robert Kyagulani maarufu kama Bobi Wine ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 3,475,398 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote zilizopigwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari 14 mwaka huu.
Pia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli amempongeza Museveni kwa kutangazwa kuwa mshindi na kusema kuwa Tanzania itaendeleza urafiki na nchi hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi.
“Nakupongeza Mhe.Yoweri Kaguta Museveni kwa kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda kuwa mshindi wa kiti cha Urais. Tanzania itaendeleza urafiki na undugu wetu kwa maslahi mapana ya wananchi. Hongera Waganda kwa kukamilisha Uchaguzi Mkuu, endeleeni kudumisha amani na upendo”. Ameandika Rais Magufuli katika ukurasa wake wa Twitter.
No comments:
Post a Comment