HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2021

MHANDISI KASEKENYA AWAPONGEZA UCHUKUZI KUKUZA VIPAJI

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akionesha umahiri wake katika kuuchezea mpira kwa kichwa baada ya kuzinduwa rasmi Bonanza la Sekta ya Uchukuzi lililofanyika katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam.

 

 Na Mwandishi Wetu


NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameipongeza sekta ya Uchukuzi kwa kukuza vipaji katika michezo na hivyo kuiletea heshima Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika mashindano ya kitaifa.

 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua Bonanza la Sekta ya Uchukuzi, Naibu Kasekenya amesema michezo licha ya kuburudisha na kuwaweka watu karibu hujenga afya ya mwili na akili na hivyo kuleta tija mahali pa kazi.

 

"Nawataka wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza michezo na kuibua vipaji miongoni mwa watumishi ili kuwawezesha kuwa wenye afya njema na kufanyakazi kwa bidii," amesema Mhandisi Kasekenya.

 

Aidha ameitaka kamati ya maandalizi kuhakikisha Bonanza  la Tano linafanyikia mjini Dodoma ili kuongeza idadi ya washiriki.

Naye Mwenyekiti wa maandalizi ya bonanza hilo, Bw. Alphonce Mwingira amesema uwepo wa tamasha hilo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamuriho, kuhusu umuhimu wa michezo mahali pa kazi ili kujenga umoja na ushirikiano. 

 

Mbali na michezo na burudani, katika bonanza hilo washiriki pia walipata fursa ya kupima afya zao na kupata ushauri wa kitabibu.

 

Zaidi ya taasisi 14 za sekta ya Uchukuzi, zikiwemo TAA, TMA, TCAA, LATRA, TASAC, TAZARA, TRC, TPA, KADCO, ATCL, MSCL, SINOTASHIP, NIT na DMI zimeshiriki bonanza hilo lilokuwa na michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, pete, kuvuta kamba, mpira wa wavu, kucheza bao na riadha.

No comments:

Post a Comment

Pages