HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 27, 2021

WAFANYABIASHARA WA MATUNDA WAGOMA KUSHUSHA MZIGO SOKO LA NDUGAI

 

Baadhi ya wafanyabiashara ya matunda wakiwa wanashusha bidhaa hizo katika soko la sabasaba badala ya kushushia katika soko Kuu la Ndugai Kama uongozi wa Jiji unavyoelekeza.


NA DANSON KAIJAGE, DODOMA


WAFANYABIASHARA ya matunda katika soko la Sabasaba Jijini Dodoma wamesema hawapo tayari kushusha bidhaa hizo katika soko Jipya la Job Ndugai lililopo Nzuguni Jijini hapa.

Wamesema sababu kubwa ya kutokubaliana na uongozi wa Jiji wa kushusha matunda katika soko la Ndugai ni kutokana na soko hilo kutokuwa na nafasi kubwa ya kushusha mzigo na kukosekama kwa eneo la kuuzia.

Kutokana na hali hiyo wameuomba uongozi wa Jiji  kuwapatia eneo lenye hadhi ya kushusha matunda hayo na eneo hilo liwe na uwezo wa kuweza kushusha mzigo na kuuza mzigo kama ilivyo katika soko la sabasaba ambapo wanashushia mzigo hadi sass.

Ombi hilo mimekuja ikiwa muda mfupi upngozi wa halmashauri ya Jijiji la Dodoma kuwataka wafanyabiashara hao kushusha mizigo yao ya matunda katika soko jipya la Job Ndugai lililopo Nzugini Jijini hapa.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Matunda katika soko la Sabasaba leo 26 Januari 2021 wamesema kuwa wanakumbana na adha kubwa ya kufanya biashara ya matunda sambamba na kupata hasara kutokana na kutokuwa na utulivi wa uhakika katika kushusha mizigo.

Kutokana na hali hiyo mmoja wa wafanya biashara aliyejitbulisha kwa Jina la Denis Athumani maarufu kwa jina la White amesema kwamba wafanyabiashara wa matunda wamekuwa wakifanya biashara yao kwa munyanyaswa na viongozi wa Jini na kusababisha wafanyabiashara hao kupata hasara.

White amesema kuwa wafanya biasjara ya matunda wamekuwa wakilazimishwa kuweka na kushisha biashara ya matunda katoka Job Ndugai ambapo hakuna miundombinu rafiki.

Wakizungumza na vyombo vya habari wafanyabiashara hao wamesema kuwa wanasikitishwa na hatua ya viongozi wa Jiji kuwafafanya wauza matunda kama sehemu ya wafanya biashara haramu.

"Kinachotushangaza sisi wafangabiashara wa matunda ni viongozi wa Jiji kutunyanyasa na kutupa masharti magumu ya kushusha mzigo katika soko jipya la Jopo Ndugai lililopo Nzuguni jijini hapa.

"Wakati huo huo wafanyabiashara wa Nafaka,Vifaa vya ujenzi na vyakula kwa ujumla magari yanashushia bidhaa hizo mjini,inakuwaje sisi wafanyabiashara wa matunda ndotunalazimishwa kushushia biashara yetu huko mbali"amehoji white.

Kwa upande wake Mabeyo Daud ambaye naye ni mfanyabiashara wa matunda amesema anaiomba serikali kwa maana ya Waziri Mkuu au Rais kuingilia kati mgogoro huo kati ya wafanyabiashara wa matunda na uongozi wa Jiji la Dodoma.

"Napa tunaposhushia matunda tumepewa na Jiji kwa utaratibu na makubaliano ya kujaza kifusi ili pasiwe na hali mbaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na tumefanya hivyo.

"Tumemwaga vifusi na kutengeneza kwa umoja wetu na mpaka sasa tunadaiwa laki saba na waliotusombea kifusi,walituambia tusiingize nagari zaidi ya tani tatu na tumetekeleza na wametupa masharti kuwa magari yasiingie kushusha mzigo katika soko la sabasaba bila kupitia stendi ya Ndugai na kulipa ushuru wa stend sh.15000 kila gari ya matunda na tunafanya hivyo sasa wanapotuchosha ni pale wanapotugeuka na kutuona Kama hatufahi"amesema Mabeyo.

Hata hivyo wamesema kuwa wapo tayari kuhamia katika soko la Ndugai kama Jiji linavyopenda, lakini wakasema ili kuhamia huko wanahitaji mambo yafuatayo.

Wameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kuwataka wafanyabiashara wengine kama wauzaji wa nafaka,vifaa vya ujenzi pamoja na bidhaa nyingine nao washushe stendi kuu ya Ndugai, pia wamesema ili waweze kushusha matunda karibu na stendi hiyo wanatakiwa kupewa eneo kubwa ambalo wataweza kushusha mzigo na kupata maeneo ya kuuzia.

"Tunaomba serikali iangalie kwa jicho la karibu na lautambuzi kuwa wafanyabiashara wa mali mbichi (matunda) wanafanya biashara ambazo haziitaji usimbufu na nirahisi kukata mtaji wao"ameeleza Mabeyo.

Kwa upande wake Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma James Yuna amesema lengo la uongozi wa Jiji siyo kuwanyanyasa wafanyabiashara wala kuwasababishia hasara bali ni kuwatengenezea mfumo mzuri wa kibiashara.

"Hili ni Jiji na tunawahitaji sana wafanyabiashara wote bila wa matunda,mbogamboga mkubwa wala mdogo lengo ni kuwajengea miundombinu na ufaratibu mzuri wa kufanya biashara katika maeneo rasmi"ameeleza Ofisa Masoko Yuna.

No comments:

Post a Comment

Pages