HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 27, 2021

Ewura yasitisha zoezi la kutoa Ankara za maji katika mikoa yote ya Tanzania Bara


Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa EWURA  mhandisi Godfrey Chibulunje, akizungumza na waandishi wa habari. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

  NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

MAMLAKA  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesitisha  upandishaji wa Ankara za  maji Mamlaka za maji na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2021 na badala yake wametakiwa watumie za mwaka 2018/2019 hadi hapo itakapotangazwa tena katika  mikoa yote  ya Tanzania bara na .
 Hayo yamesemwa hii leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa EWURA  mhandisi Godfrey Chibulunje wakati akizungumza na waandishi wa Habari.

 Amesema malalamiko yamekua mengi   juu ya maji na wengi wanalalamikia kuhusu kubambikiwa ankara za maji.

"asilimia 75 ya malalamiko ni ankara za maji kuwa kubwa lakini pia asilimia 13 za malalamiko ni migogoro ya uunganishwaji  wa upatikanaji maji na kuchelewa kwa  huduma Kwa wananchi  " amesema Mhandisi Chibulunje.

Amesema Kutokana na hayo Ewura huainisha bei kwa mamlaka za maji za miaka mitatu ambazo bei nyingi ziliainishwa Kwa mwaka 2018 /2019 , 2019/20 na 2020/21 na ambao zilikuwa zinaendelea  kutumika.

"kwa mujibu wa utaratibu huo kuanzia january 2021 mamlaka nyingi zilikua zinatarajia kuanza kutumia bei za mwaka 2020/21  hivyo basi kutokana na malalamiko hayo  yaliyofafanuliwa Ewura imefuta bei zote  ambazo zilitakiwa kuanza kutumika kuanzia january 2021 na mamlaka ya maji  zote zitaendelea kutumia bei za maji za mwaka 2018/2019 "amesema Chibulunje.

Amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuipa uwezo ewura kufanya uchunguzi wa kina juu ya malalamiko hayo ya maji ili kubaini ukweli wa malalamiko hayo.

 Hata  hivyo  amesema kuwa baada ya kumaliza kufatilia shughuli za uchunguzi wa kiufundi Ewura itatoa matumizi mengine ya bei ambazo zilitakiwa kuanza january 2021 na hii ni kwa mikoa yote ya Tanzania .

No comments:

Post a Comment

Pages