Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo, Sylvia Chaula (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Upendo Wote Kwako” itakayohamasisha wateja wa benki hiyo, kutumia huduma za MB Mobile na mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji na Teknohama wa benki hiyo, George Wandwalo na Mratibu wa kampeni hiyo, Elinipendo Mziray.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo, Sylvia Chaula (katikati), akizindua kampeni ya 'Upendo Wote Kwako' itakayohamasisha wateja wa benki hiyo, kutumia huduma za MB Mobile na mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao.
Na Mwandishi Wetu
MAENDELEO Bank imezindua kampeni ya ‘Upendo Wote Kwako’ inayolenga kuhamasisha wateja wa benki hiyo kutumia huduma za MB Mobile pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Meneja Huduma kwa Wateja wa Maendeleo Bank, Sylvia Chaula, alisema kuwa kampeni hiyo imeanza Februari 4 Februari na kilele chake itakuwa siku ya wapendanao (Valentine Day) Februari 14 ambapo washindi wa watatu watakaoshinda watapa zawadi mbalimbali ikiwemo Laptop, Simu Janja, Saa pamoja na kupata chakula cha usiku na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Dk. Ibrahim Mwangalaba pamoja na jopo la wafanyakazi wa benki hiyo katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo jijini Posta Kijiji Dar es Salaam.
“Washindi wote watatu watapata nafasi adhimu ya kuwaalika wapendwa wao katika chakula cha usiku, yaani kila mshindi atakuja na mwenza wake katika siku hiyo ambapo pamoja na chakula cha usikupia kutakuwa na tukio la washindi kupokea zawadi zao kutoka kwa Maendeleo Bank”. Alisema Sylvia.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo Uendeshaji na Tehama wa benki hiyo, George Wandwalo alisema kuwa “Siku hiyo ya wapendanao sisi kama Maendeleo Bank tutatumia muda watu kuwaonyesha wateja wetu kama tunawapenda, tunawajali na kuwathamini ndio maana tumechagua siku hiyo kuwaonyesha upendo walionao kwao kwa vitendo na si maneno.”
Maendeleo Bank imeendelea kawa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma za kuja na majawabu mbalimbali yanayoweza kuwakwamua watu kiuchumi na hivyo kutoka kwenye hali moja ya maisha na kwenda kwenye hatua nyingine, Maendeleo Bank imekuwa ikifanya hivi kwa kuja na huduma mbalimbali kama vile huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo, wafanyakazi, taasisi, vikundi na huduma nyingine nyingi za kibenki.
No comments:
Post a Comment