HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 06, 2021

TAKUKURU YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUMISHI 11 KWA UFUJAJI FEDHA-BUKOBA

 


Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, John Joseph.

  

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani kagera imewafikisha mahakamani  watumishi 11 wa halmashauri ya Biharamulo mkoani humo, kwa tuhuma za ufujaji fedha zaidi ya shilingi milioni 640.

Watuhumiwa hao  ni pamoja na afisa kilimo, maofisa watendaji, mhudumu wa hospitali, afisa afya, pamoja na mhasibu wa mapato Biharamulo.

Mwanasheria wa mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Kagera Domick Maganga, amesema kuwa kati ya watuhumiwa hao 11, ni mmoja tu aliyetimiza masharti ya dhamana na mashauri yatatajwa tena kati ya tarehe 15,16,17/02/2021, na kesi ya mmoja aliyepata dhamana itatajwa tena tarehe 04/03/2021.

Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU mkoani Kagera John Joseph, amesema kuwa uchunguzi ulifanyika mwaka jana baada ya kubainika kuwa watumishi wa kada mbalimbali wamefuja fedha za makusanyo ikiwemo zilizokusanywa kwa njia ya posi na wengine kutotumia mfumo huo.

 Aidha watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani baada ya TAKUKURU kubaini shilingi milioni 645,214,000 zilikuwa zimefanyiwa ubadhirifu na baadhi ya watumishi Julai 2018 hadi Juni 2020, kupitia mfumo wa makusanyo ya serikali yaani posi.

No comments:

Post a Comment

Pages