NA VICTOR MASANGU, MAFIA
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amepokea kivuko kipya kilichopewa jina la Mv Kilindoni – Hapa kazi tu kilichogharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.3 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa lengo la kuwaondolea wananchi wa Wilaya ya Mafia adha ya usafiri ambayo walikuwa wanakabiliana nayo.
Injiani Ndikilo amepokea kivuko hicho kwa niaba ya Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Mh. Injnia Leonard Chamuriho wakati wa sherehe ambazo zilifanyika katika visiwa vilivyopo Wilayani Mafia na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali. Wakuu wa taasisi mbali mbali pamoja na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi sambamba na wananchi .
Mkuu huyo alisema kwamba kivuko hicho ni moja ya ahadi ambazo zilitolewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa lengo la kuweza kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Mafia na maeneo mengine waweze kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya usafiri wa majini ambao ulikuwa unawasumbua kwa muda mrefu.
Pia alifafanua kwamba kivuko hicho amabcho kina uwezo wa kubeba abiria wapatao 200 pamoja na tani 100 za mizigo kinatarajia kuanza kufanya safari zake rasmi siku ya kesho jumanne ambapo kitakuwa kinawabeba wananchi mbali mbali kutoka eneo la Nyamisati na kuelekea katika eneo la kilindoni Wilayani Mafia na kwamba ujenzi wa kivuko huo umefanywa na Songoro Marine Trasport Boatyard LTD ya Mwanza.
“Kivuko hiki kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.3 na kwamba fedha hizi zimetolewa na Rais wetu Mpendwa hivyo tunampongeza sana kwa ahadi yake na kwamba hapo awali wananchi wa mafia bado walikuwa na changamoto ya usafiri wa majini japo kuna kivuko kingine kilikuwepo cha mtu binafsi amabcho nacho kimeweza kusaidia sana wananchi na hiki cha serikali kina uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 100 za mizigo,”alifafanua Ndikilo.
Katika hatua nyingine Ndikilo alisema kwamba kivuko hicho pia kitaweza kufungua fursa za kiuchumi kutokana na wananchi wa Mafia kuweza kuendesha shughuli zao mbali mbali za uzalishaji mali na biashara na kuwahimiza waweze kuwa walinzi wazuri katika kukitunza kivuko hicho amabcho walikuwa wakikisubilia kwa shauka kubwa.
“Asante sana Mh. Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli kwa kwa kuweza kutekeeleza ahadi yako ya kuleta kivuko hicho ambacho kitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Mafia na kufungua zaidi fursa za wananchi wengine katika kufanya biashara,”alisema Ndikilo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno pia ametoa pongezi zake za dhati kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweza kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kivuko hicho ambacho ameeleza kuwa kitaweza kuwa ni moja ya kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Wialya ya Mafia mkoani Pwani na maeneo mengine.
Nao baadhi ya wananchi Wilayani Mafia ambao wamehudhulia katika sherehe hizo walisema kwamba hapo awali walikuwa wanakabiliwa na changamoto katika suala zima la usafiri hivyo kukamilika kwa kivuko hicto kitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kufanya shughuli zao na kuleta maendeleo.
“Kwa kweli sisi kama wananchi wa ya Mafia tunapoa shukrani zetu kwa Rais wetu Mpwendwa kwa kuweza kutujali na kutuletea kivuki hiki ambacho kinajulikana kama ,Mv Kilindoni na kwamba kitakuwa ni moja ya kutataua changamoto za usafiri na kitarahissha zaidi utaekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku na kukuza uchumi zaidi.”walisema wananchi hao.
Wananchi wa Wilani Mafia Mkoa Pwani wamekuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya siku nyingi ya adha ya usafiri wa majini hivyo kukamilika kwa kivuko hicho cha Mv kilindoni – Hapa kazi tu kutaweza kuleta mabadiliko makubwa hasa katika Nyanja mbali mbali za kukuza uchumi, pamoja na wananchi kupata futrsa ya kuendesha biashara zao mbali mbali ikiwemo kuwavutia wawekezaji.
No comments:
Post a Comment