NA SULEIMAN MSUYA
VIONGOZI
wapya wa Kundi la Simba Jamii Tanzania Enterprises (SJTE) wameahidi
kufanya kazi kwa uadilifu, uwajibikaji, nidhamu na maadili kuhakikisha
wanaifikisha mbali taasisi hiyo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari baada ya kuchaguliwa baadhi ya viongozi hao
katika uchaguzi uliofanyika jijini Dar es Salaam January 31, 2021
walisema wamepokea kijiti hivyo wanawajibu wakufanya makubwa zaidi kwa
(SJTE).
Mwenyekiti mpya
wa SJTE, Patrick Mwanakatwe amesema anashukuru wana Simba Jamii
kumuamini na kumchagua hivyo atahakikisha hawaangushi.
"Awali
ya yote napenda niwashukuru sana kwa kuweza kuniamini na kunichagua
kuwa Mwenyekiti wenu wa SJTE. Nawaahidi nitakuwa bega kwa bega nanyi
katika kuiendeleza taasisi ilituweze kufikia malengo tuliyojiwekea.
Niwapongeze
viongozi waliomaliza muda wao kwa kutuanzishia msingi mpaka hapa tulipo
ni mengi mmepitia nawaahidi kushirikiana nanyi popote pale tutakapo
omba msaada.
Nawaomba
msisite kutupa ushauri pale tunapoomba ushauri kwani sisi sote ni
wanachama wa SJTE wote tupo ndani ya mtumbwi moja na nahodha wetu ni
mmoja mtumbwi ukizama tunazama wote," amesema.
Mwanakatwe
amesema anawaomba wanachama wote wawe wamoja na kuondoa tofauti zao
wawe na upendo, mshikamano kwani baba yao ni mmoja na moto wao uwe ni
upendo.
Mwenyekiti huyo amesema iwapo uadilifu, uwajibikaji, nidhamu na upendo vitatawala ni wazi kuwa SJTE itasonga mbele.
"Mambo
ya nje ya group tofauti zetu tuzimalizie huko huko tukija ndani ya
group tuwe na umoja na upendo ndiyo tutafika mbali siyo mwenyekiti
nimekwazana na makamu wangu tunayaleta kwenye kundi.
Masuala
yetu binafsi tuyamalizie huko huko ndani ya kundi hapana. Nitakuwa
mkali mimi na uongozi wangu hatutaruhusu tofauti zetu tuzimalize huko
huko nje ya kundi na kama umekuja kuniomba usuluhishi basi umekuja
kwangu kama Mwanakatwe siyo mwenyekiti fahamu kuwa mimi ni mwenyekiti
wa SJTE siyo mwenyekiti wa nyie wawili," amesema.
Mwanakatwe amesema anawashukuru kwa kumchagua hivyo anawaomba wamalize tofauti zote za nyuma na kuzizika.
Aidha
Mwenyekiti amesisitiza wanachama walipe ada kwa mujibu wa Katiba na kwa
wakati na sio kusubiri kusukumana kwani nisheria na kanuni za SJTE
zinaelekeza ulipaji.
Poa
Mwanakatwe amesisitiza wana SJTE kuendeleza utamaduni wa kuchangiana
wakati wa shida na raha kwani ni moja ya kiashiria cha upendo.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa SJTE, James Tindi amesema taasisi hiyo
itafikia malengo iwapo mshikamano utakuwepo baina yao.
Tindi amesema matamanio yake ni kuona kundi hilo lina linakuwa chachu ya maendeleo, uchumi na fursa nyingine muhimu kwao.
"Uamuzi wenu wa kutuamini tutahakilisha tunalipa hivyo niwaaahidi kuwa tumedhamiria kuipeleka mbele SJTE," amesema.
Naibu
Katibu Mkuu wa SJTE, Asha Kigundula amesema atahakikisha anatumia
ushawishi wake kuchochea mafanikio ndani ya taasisi hiyo.
Amesema
SJTE inatakiwa kufikia kwa wadau kwani ni moja ya kundi la washabiki na
wanachama wa Timu ya Simba ambalo lina malengo tofauti na ushabiki.
Akizungumza
baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi SJTE, Rahim
Varisanga amewataka wanachama wote waliochaguliwa kutambua kuwa wana
deni kubwa kwa wanachama.
Varisanga
amewataka viongozi wapya wa SJTE kufuata misingi ya uongozi kwa
kuvumilia mabaya yote ambayo watakutana nayo kwani ndio sababu ya
migogoro.
"Niwapongeze
wagombea wote kwa nafasi ambazo mmepata ilanataiwa kutambua kuwa
mmepokea dhima kubwa ya watu mnatakiwa kuwa kitu kimoja ili SJTE ifikie
malengo," amesema.
Katika
uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa kuzingatia utaratibu zote pia
wagombea wengine walichaguliwa ni Katibu Mkuu Hassan Mohammed, wajumbe
wa Kamati ya Utendaji Nunu Mbegu, Mussa Rashid na Laurencia Sahani.
No comments:
Post a Comment