Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa akitoa maelezo mafupi katika ziara hiyo kuhusu mradi wa ujenzi wa bwawa ambalo linajengwa kwa ajili ya kunyweshea mifugo mbai mbali katika kijiji cha cahamakweza. (Picha na Victor Masangu).
Mkuu wa Mkoa wa Pwani MhandisiEvarist Ndikilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya mkoa akitoa ufafanua kwa wananchi pamoja na jamii ya wafugaji na wakulima wa kijiji cha cahamakweza wakati wa ziara hiyo yenye lengo la kuwasikiliza kero na changamoto zao.
Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Pauline Gekul wakti akizungumza jambo na baadhi ya wafugaji na wakulima katika kijiji cha Chamakweza na pingo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuwatembelea wananchi hao pamoja na kuweza kusikiliza changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili ili kuzifanyia kazi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwasalimia wananchi pamoja na baaadhi ya jamii ya wafugaji na wakulima ambao waliweza kufika katika ziara hiyo ambayo ilikuwa inalenga kusikiliza changamoto zao pamojaa na kujionea miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa bwawa kubwa kwa ajili ya kunyeshea mifugo.
Baadhi ya jamii ya wafugaji wanaofanya shughuli zao katika kijiji cha chamakweza wakiwa wametulia kwa umakini kwa ajili ya kuwasikiliza viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambao walifanya ziara kwa ajili ya kusikiliza changamoto zao ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
NA VICTOR MASANGU, CHALINZE
KUFUATIA kuwepo kwa wimbi la mapigano kila kukicha kati ya jamii ya wakulima na wafugaji katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo halmashauri ya Chalinze na kusababisha hali ya uvunjifu wa amani serikali ya awamu ya tano imekuja na mpango wa kukomesha hali hiyo ambapo imedhamilia kutatua na kumalizaka kabisa migogoro ipatayo 40 ambayo tayari imekabidhiwa katika Wizara husika.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Pauline Gekul wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea mradi wa lambo kubwa la kunyweshea mifugo pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi katika vijiji vitatu vya vya Chamakweza, Ruvu darajani na kijiji cha Kitonga vilivyopo katika halmashauri ya Chalinze.
Aidha Naibu Waziri huyo aliwataka jamii ya wafugaji na wakulima wote katika maeneo mbali mbali ya halmashauri ya Chalinze kwa sasa kuwa watulivu na wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote za nchi ikiwemo kuheshimiana wakati serikali inaendelea na juhudi za makusudi katika kulitaua jambo hilo la mgogoro uliokuwepo ili amani iweze kurejea.
“Nimepokea katika Wizara yangu migogoro ipatayo 40 na hii inahusina na mambo haya haya wa migogoro katika ya wakulima na wafugaji na vijiji hivi vya chamakweza pamoja na pingo na maeneo mengine ni moja ya sehemu ambayo na yenyewe ipo katika mvutano huu lakini mimi nina waahidi kulimaziza suala hilo na uzuri limeshafika katika mamlaka zinazohusika wala sio kwa Mkuu wa Mkoa tena.,”alifafafanua Naibu Waziri huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amebainisha lengo la serikali ni kuhakikisha inazifuatilia fedha ambazo zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ili kujionea kama ipo katika kiwango kinachotakiwa na kuwataka wafugaji na wakulima kumaliza kabisa migogoro na mapigano yao na kuachana na kufanyiana vitendo vya ubaguzi.
Mmoja wa wa wafugaji akisoma tamko lao ambalo wameliandaa mbele ya Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi kwa niaba ya wenzake amebainisha kwamba kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi ya wakulima kufanya uvamizi katika maeneo ya marisho na kuamua kuyauza kinyemela kwa watu kutoka maeneo mbali mbali.
Naye Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa katika jambo ambalo wamekuwa wakilipigia kelele kwa kipindi kirefu ni mradi wa ujenzi wa lambo hilo kwa ajili ya mifugo na kwamba ameipongeza serikali ya awamu tano kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 700.
“Kwa kweli kwa uoande wangu mimi kama Mbunge wa Jimbo la Chalinze nipende kumshukuru Rais wetu wa wamau wa tano kwa kuweza kututhamani sisi wananchi kukubali kutoa kiasi cha shilingi milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu wa bwawa kubwa katika kijiji hiki cha chamakweza na litaweza kuwa mkombozi mkubwa wa mifugo yetu,”alisema Mbunge Huyo.
Pia alisema kwamba ni kweli kumekuwepo kwa changamoto kubwa kwa wakulima na wafugaji katika baadhi ya maeneo ya vijiji hasa katika eneo hilo la wananchi wa vijiji vya Chamakweza na pingo lakini anashukuru viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Naibu waziri wa mifugo na uvuvi kufanya ziara maalumu kwa ajili ya kwenda kutafuta ufumbuzi.
HALMASHAURI ya Chalinzie Iliyopo Wilayani Bagamoyo imekuwa ikikabiliwa na chanagmoto kubwa katika baadhi ya vijiji vyake kuwepo kwa migogoro kila kukicha na mapigano kati ya wakulima na wafugaji kutokana na kugombania maeneo ya mipaka ya ardhi hivyo na kusababisha vurugu hivyo jitihada ambazo zimefanywa na serikai ya awamu ya tano zitaweza kuleta matokeo chanya ya kumaliza vurugu hizo.
No comments:
Post a Comment