HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 10, 2021

UTT AMIS YASHIRIKI MAONYESHO YA MIFUKO YA UWEZESHAJI, KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOZUIA WANANCHI KUWEKA AKIBA

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho   ya Nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi  kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mmoja wa wananchi akipata huduma katika banda la Kampuni ya UTT AMIS.
Wawakilishi wa madiwani kutoka kata za Arusha Mjini wakiwa katika banda la UTT AMIS.
 
 
Arusha, Tanzania 
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Jumanne, Februari 9, 2021  amefungua Maonesho ya Nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi yanayoendelea katika Viwanja vya Shiekh Amri Abeid jijini Arusha.

Katika ufunguzi huo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza mifuko na programu zote za uwezeshaji zifanye tathmini ya shughuli na huduma zake ili kubaini mafanikio, changamoto na maeneo yanayohitaji uboreshaji hususan eneo la masharti ya utoaji mikopo kwa wajasiriamali.

Amesema tathmini za mara kwa mara zinazofanywa na Serikali kuhusu utendaji wa Mifuko na Program za Serikali za uwezeshaji zinaonesha kwamba mifuko hiyo na programu hizo zimechangia kwa kiwango kikubwa jitihada zake za kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa amesema baraza hilo linajukumu la kusimamia, kufuatilia na kuratibu shughuli mbalimbali za uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo mifuko na programu za uwezeshaji.

“Mifuko hii imeanzishwa kwa ajili ya kutatua changamoto zinazozuia wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, ambazo ni pamoja na ufinyu wa vyanzo vya akiba na mapato, kutokuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba,” amesema.

Amesema, baraza linaratibu mifuko na programu za uwezeshaji zipatazo 55, ambapo kati yake mifuko ni 48 na programu saba. Uratibu unaofanywa ni pamoja na kutunza daftari la orodha ya mifuko, kufanya mikutano na taasisi zenye mifuko na programu za uwezeshaji, kupokea taarifa za mifuko na kujenga uelewa kwa umma juu ya uwepo wa mifuko na programu hizo. 

No comments:

Post a Comment

Pages