HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2021

Waliokula hela za ukarabati jengo la Posta watakiwa kuzirejesha

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Habari na Teknolojia Mhandisi Kundo Andrea, akionesha taa iiyowekwa kuwa ni ya kawaida lakini gharama yake iko juu na haiendani na taratibu za manunuzi.

 

NA IRENE MARK
 
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Mhandisi  Kundo Andrew, ameuagiza uongozi wa Shirika la Posta Tanzania kurejesha zaidi ya Sh. Milioni 600 walizotumia vibaya kwenye ukarabati wa jengo la Posta jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Kundo alisema amebaini ubadhirifu kwenye ukarabati wa jengo hilo baada ya kufanya ziara ya ghafla kwenye makao makuu ya Shirika la Posta na kuthaminisha ukarabati na fedha zilizodaiwa kutumika.

“Huu ni ubadhirifu wa fedha umma kwenye ukarabati wa jengo la Shirika la Posta... tunaambiwa zilizotumika ni Sh. Bilioni moja. Nimekagua thamani ya fedha haipo.
 
“Mheshimiwa Rais John Magufuli anapambana kupata fedha kwa ajili ya wananchi wanyonge lakini baadhi ya watumishi wanafuja fedha hizo kwa ukarabati usioendana na thamani ya fedha kutokana na shirika hilo kushindwa kusimamia na kusababisha mkandarasi kulipua kazi,” alisema Mhandisi Kundo.
 
Kwa mujibu wa Mhandisi Kundo, ukarabati wa jengo hilo umegubikwa na usanii mwingi huku akutaja thamani halisi ya ukarabati huo kuwa ni Sh. Milioni 400 badala ya Sh. Bilioni moja kama inavyoelezwa na wakuu wa Shirika la Posta Tanzania.
 
Amesema kuwa kwa mradi wa ukarabati wa jengo hilo thamani halisi ni sh.milioni 400 hivyo sh.milioni 600 lazima zirudi ili ziweze kufanya kazi hata kujenga daraja au hospitali kwani wananchi bado wanashida hivyo vitu.
 
Naibu Waziri huyo amesema katika kipindi hiki hakuna mtu ataachwa salama ikiwemo Posta  kwa fedha iliyofanya ukarabati isioendana na thamani kabisa  huku menejimenti ya shirika ikiwa haina hata habari.
 
Aidha  amesema Meneja mkuu wa Shirika la Posta kuwa mwangalifu kusiwepo na watu wa kumzunguka kwa vitu vidogo kwani anatakiwa kuangalia baadaye kushika nyadhifa zingine kutokana na umri wake na hakuna anayetambua kuwa baadaye anaweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
 
Mhandisi Kundo amesema kuwa taarifa za shirika hilo anazo hivyo hakuna mtu wa kuweza kumdanganya katika kuficha ukarabati wa ujenzi huo na namna mkandarasi aliyepatikana katika kuchukua zabuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages