Naibu Waziri wa Tamisemi David Silinde ameagiza halmashauri ya Ndanda iliyopo mkoani Mtwara kujenga majengo mengine katika shule ya Msingi Mpowora baada kukuta madarasa mabovu kabisa ambayo yanaweza kuwaangukia wanafunzi mda wowote. Kauli hiyo ameitoa alipotembelea shule hiyo.
Kusoma
katika mazingira mazuri na yenye majengo mazuri ni moja ya kishawishi
kikubwa cha ufaulu wa wanafunzi katika mitihani yao lakini kwa wanafunzi
wa shule ya msingi Mpowora iliyopo Ndanda wilaya ya Masasi, mkoa wa
Mtwara ni tofauti kwani kwa sasa wanafunzi katika shule hiyo wanatumia
madarasa ambayo yamechoka sana huku yakiwa na nyufa ambazo
zinawajengea hofu ya kusoma na kutimiza ndoto zao.
Japhet
Anord na Shamira Bushiri ni wanafunzi wa shule hiyo wakiokba serikali
yao kutenga fedha ya kuwajengea madarasa mapya baada ya madarasa kuwa
hatarishi kwao ambayo hayana madirisha na kufanya mvua ikinyesha maji
yao,jua likiwa kali lao huku mbao zikiwa zimeliwa na mchwa na
kuwatengenezea hofu kwani mda wowote majengo hayo yanaweza waangukia.
Cecil
Mwambe ambaye ni mbunge wa Ndanda na ni mwalimu mkuu wa shule hiyo
wameiangukia serikali kuisaidia shule kwa kujengewa madarasa mapya kwani
kwasasa hali ni mbaya zaidi huku walimu wa shule hiyo wakikosa vyoo vya
kujisaidia na kuomba mkono wa serikali na wananchi wapo tayari
kuchangia.
Kwa upande wa
serikali kupitia kwa Naibu waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI David
Silinde ambaye alifika shuleni hapo kujionea mazingira wanayosomoa
wanafunzi hao na kuahidi kuingiza fedha kiasi cha milioni 40 siku hiyo
ambayo ni nje ya bajeti na kuwaahidi wanafunzi na walimu kuwa shule hiyo
itaingizwa katika bajeti ya kuwajengea madarasa mengine mapya na kuwa
yeye hajaridhika kabisa na mazingira ya wanafunzi wanaposomea.
No comments:
Post a Comment