NA HAMIDA RAMADHANI DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya kilimo imefanya kikao cha pamoja na wadau wa kilimo kuhusu mradi wa miaka mine wenye thamani ya Euro Milioni 100.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
Naibu
Waziri huyo Bashe amesema lengo la kikao kazi hicho na Wadau wa kilimo
ni kuangalia maeneo gani uwekezaji wa fedha unahitajika zaidi .
Aidha, Bashe amesema sehemu kubwa ya fedha katika mradi huo wa miaka minne inaenda kwenye miundombinu ya barabara ambapo ni Euro Milioni 48 .
"Nasisitiza kupunguza gharama za utawala na gharama za semina ili kuwekeza zaidi kwenye miundombinu," amesema Naibu Waziri Bashe
Kwa
upande wake mratibu mradi wa MARKUP Safari Fungo amesema wamejikita
zaidi katika kusaidia taasisi za kilimo kutafuta masoko na kuvutia
mitaji kutoka nje ili kuvutia wawekezaji.
Mradi huo wa miaka mine unaofadhilia na umoja wa Ulaya unaratibiwa na Taasisi ya MARKUP,AGRICOM,SELFIER na SOLIDAT .


No comments:
Post a Comment