CHAMA Cha ACT Wazalendo kimewataka wanachama na wananchi pamoja na wapenzi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania marehemu John Pombe Magufuli unaotarajiwa kuwasili Zanzibar Machi 23.
Kauli hiyo imetolewaa na Katibu wa habari na Uenezi wa chama hicho Salim Bimani wakati akizugumzza na waandishi wa habari katika ofisi ya chama hicho iliyopo Vuga Mjini Unguja.
Bimani alisema Zanzibar ni Sehemu ya Muungano wa Tanzania na wananchi wake wanawajibu wa kumuaga kiongozi wao ambae alilitumikia taifa muda wote katika uhai wake.
“Teendeni tukamuage kiongozi wetu hakika atika uhai wake alipambana sana katika kuijenga Tanzania” alisema Biman
Aliwataka wahusika wa maandaizi ya kuwaleta watu Mjini kutoka maeneo ya mashamba kufanya jambo hilo bila kingiza misimamo ya kisiasa ili wazanzibar wote wapate nafasi hiyo.
“Tayari Serikali imetuahidi kuwa watawaleta watu 200 kutoka kisiwa cha Pemba ambao watachuwa watu wote bila kujali misimamo ya kisiasa” alisema Biman.
Hayati John Pombe Magufuli atakumbukwa kwa mengi alikua ni mtu mwenye kutamani maendeeo na alikuwa na hamu ya kuiona Tanzania inafanya mabadiliko.
“Tunamkumbuka kwani alikuwa akiamini na kukisimamia miraadi mingi aliyoianzisha na kuitekeleza” alisema Bimani.
“Pia tutamkumbuka kwa kuanzisha Miradi mikubwa ya mabarabara na madaraja njia za reli usafiri wa anga kwa kunua ndege,kupiga vita rushwa na uhujumu uchumi,kupiga vita ubadhirifu wa mali za umma na wizi”alisema Biman.
Hata hivyo walisema watamkumbuka kwa kutaka kuona Tanzania inakuwa na mabadliko makubwa katika kila Nyanja na aliahdi kuondoa kabisa ufisadi ili nchi iwe katika hali yake ya heshma.
Kwa upande wa Rais Samia Kiogozi huyo alisema anamini kushika wadhifa wa Urais mama Samia Suluh Hassan ataliunganisha taifa la Tanzania na kulirudisha katika umoja wake
Hata hivyo amemuomba mama Samia kushughulikia mkwamo wa katiba pendekezwa ili aweza kulijega taifa ambalo wananchi wanalitamani,
Smbamba nah lo Bimani alimtaka Rais Samia kurudisha umoja na ushirikiano baina ya vyama vya Upinzani ambao kwa kipindi uliyumba.
“Tuategemea Rais wetu atasimamia vyema majukumu yake ili kuikwamua Tanzania pale ilipokwama” alisema.
Wakati huo huo Bimani alisema kesho siku ya Jumatatu uongozi wa ACT wazalendo ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Juma Duni Haji watakwenda kusaini kitabu cha Maombolezo na Baadae kufika Kisiwa Ndui kwenye Afisi Kuu ya CCM kutoa mkono wa Pole kwa vongozi wake ambao walifiliwa na Mwenyekiti wao.
“Sisi tulipofiliwa na Mwenyekiti wetu wenzetu walikuja kutufariji na sisi hatuna budi wenzetu kuwafariji kwa kuondokewa na mwenyekiti wao” alisema Biman.
Tunampa Pole Rais wa Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi. Viongozi wa CCM pamja na Familia ya Hayati John Pombe Joseph Magufuli.
No comments:
Post a Comment