Chama cha Waandishi wa Wahabari Wanawake Tanzania,
Zanzibar, (TAMWA ZNZ) kinampongeza, Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa
awamu ya sita wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa
mwanamke wa kwanza nchini Tanzania na Afrika Mashariki kushika nafasi ya
hiyo.
Uteuzi huo umetokea baada ya msiba wa
aliyekuwa Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli kufariki dunia hapo
Machi 17 mwaka huu ambao TAMWA ZNZ imesikitishwa na msiba huo.
Rais
Samia kwa hiyo kama inavyoelekeza katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kifungu 37 (5) ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ushindi mkubwa kwa jitihada za miaka mingi za
ukombozi wa wanawake hapa nchini.
Kuapishwa kwa Mama
Samia kuwa Rais wa Tanzania kutaweka mustakbali mpya kwa maendeleo ya
jinsia hapa nchini pamoja na Afrika Mashariki kwa ujumla na kwamba
kutatoa nuru zaidi kwa wanawake na wasichana kukwea/kupaa ngazi za
uongozi.
Tunaiomba pia jamii ya Watanzania kuondoa
mawazo mgando kwa jamii ambayo hawaamini kwamba wanawake wanaweza
kushika nafasi za juu na hivyo kuchukua fursa hii ya kumuunga mkono
Mhe Raisi pamoja na kuandaa wanawake zaidi kwenye nafasi za uongozi.
TAMWA
ZNZ inamtakia kila la kheri Mama Samia katika kipindi chake hichi
kizito kutokana na kifo cha aliyekuwa Mkuu wake wa kazi na majukumu haya
ya kuiendesha nchi katika nafasi ya juu kabisa.
No comments:
Post a Comment