HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 20, 2021

Maelfu wajitokeza kumuaga JPM


Wananchi wa Kinondoni Mkwajuni na Magomeni Morocco wakiwa wamesimama barabarani kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa kuelekea Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.


Wajasiriamali wa Mau wa Namanga mkoani Dar es Salaam wakirusha maua kama ishara ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi mkoani Dar es Salaam.

 Wakazi wa Biafra Kinondoni wakimuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa.
Wakazi wa Magomeni wakimuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa.

Wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamesimama kando ya barabara kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa mkoani Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages