Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Mji Mkongwe, Halima Ibarahim Muhammed.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar Tamwa ZNZ, Dk. Mzuri Issa Ali.
Talib Ussi, Zanzibar
Naanza kwa kupeperusha bendera ya heko: Helwa! Helwa! Maajabu ya Mwanamke Jasiri! ingawa katikati ya dimbwi la machozi ya majonzi upande mmoja, sambamba na tabasamu la matumaini ng’ambo ya pili, juu ya jukwaa la fungate ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Ni dimbwi la machovu kwa sababu ndio tegemeo katika shuhuli nyiingi za majumbani na ni tabasamu ya matumaini kwa sababu si aghlabu kukta tamaa kwa chochote kile wanachokifuatilia.
Bila shaka katika ulimwengu huu inakuwa vigumu kumkosa mwanamke kunako kila aina ya shida, majonzi, mateso, maumivu, simanzi, dhiki na shakawa; bali pia hazitoweza kuiengua jinsi hiyo katikati ya tabasamu la matumaini ili kuijenga na kuiendeleza dunia hii, hadi kuwa pahala pema pa kuishi.
Utangulizi huo (Mukadima huu) hauna budi kuchochea hamasa akilini katika kuwaunga mkono wanawake hali ambayo pia kuwaibuwa mwanamke jasiri ulimwenguni na kwa kila zama ikiwa na mifano kadhaa
Wanawake waliovuma duniani, wakasimama kidete kupigania haki za wadhulumiwa pamoja na wale ambao kwa makusudi au kwa taadi tu ya nguvu danganyifu za watawala jeuri zililenga kuyadhoofisha maisha yao.
Falsafa zote duniani zimewafika kwamba ‘picha za ulimwengu’ haziwezi kupendeza, vivutio vyote haviwezi kuvutia, burudani zote hazinogi, vionjo vyote havina ladha pasi na kuwepo mwanamke; seuze maua yatakayochanua na hatimaye kupatikana matunda mazuri au vinginevyo watoto wakazaliwa.
Ni hivi karibuni ambapo Chama Cha Wandishi Wanawake Tanzania (TAMWA) walifanya mikutano kadhaa kuelimisha umuhimu wa kuwa shirikishi na kuwapa nafasi ya uongozi wanawake Ilikuwa wakati wa maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani.
Washirki katika mikutano hiyo walizungumzia kuhusu nafasi ya uongozi kwa mwanamke na kukubaliana kuwa mwanamke anaweza na ni muhimu apewe nafasi katika ngazi zote za uongozi ili kuleta usawa, na pia kumpa nafasi ya kushiriki katika kutoa maamuzi shirikishi.
Mwanamke tokea alipoumbwa kaumbwa kuwa kiongozi hivyo ni marufuku mwanamke kukata tamaa. Ni .2025 tumejipanga na.tutaingie tena katk. Uchaguzi na kugombea nafsi katka
Almuradi dunia hii au kama wanavyoita Watashi, ‘gene pool’ haiwezi kusogea au kushuhudia mabadiliko ya dhati ulimwenguni, pindipo pakikosekana jinsi ya kike, kwani mwanamke ni mama, dada, mzazi, kitulizo cha maisha na zaidi ya hayo ndiyo njia kuu ya kupelekea maisha ya binaadamu yawezekane kupitia Qadar Yake Muumba.
Wamezoea kusema, “wanawake wanaweza pindipo wakiwezeshwa”, bali ni zaidi ya hapo kwani ujasiri wa mwanamke hauna ngao ya kuuzuia kuanzia hisia zake za mbali, sambamba na mapenzi yake yasiyokuwa na mipaka, katika siri na dhahiri.
Licha ya mtiririko mrefu wa machozi ya mwanamke unaotiririka kuelekea kila upande, Mashariki na Magharibi, Kusini na Kaskazini, hakuna ubishi kwamba furaha na matumaini ya dunia hii yanamhitaji, tena kwa kiasi kikubwa.
……………………….
Wapo walitajikana, ambao ni pamoja na akina Rudo Gaidzanwa, Mama Corazon Aquino, Monica Lewinsky, ……Getrude Mongela……. Na kwa hapa kwetu huwezi kuwapembua akina Mwalimu Ruth Meena, Leila Sheikh, Rose Hadji, Mama Majoore Mbilinyi, ….
Hawavumi lakini pia wamo majabari wanawake wanaharakati wa zama hizi, akina Mama Samia Suluhu Hassan, Dokta Mzuri Issa na Mhadisi Zena Said Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao maadhimisho ya mwaka huu yamewaachia changamoto maalum katika kuhamasisha mapambano ya kutetea haki zao, kila pembe ya dunia.
Ni kwa kiasi kikubwa, na ndivyo ilivyo, kuamini juu ya nafasi na nguvu kubwa za ushawishi wa mwanamke, kupitia kurasa za maisha ya watu, tangu zama za Adam na Eva (Hawa), ijapokuwa shetani alijaribu kupenya na kulitumia pambo la jinsi hiyo katika kuparaganya mambo; au kama wasemavyo Waswahili, “sumu imo katika vinono”.
Mapambano yote duniani yalimshuhudia mwanamke akiwepo katikati, kama siyo usoni kabisa au mstari wa mbele, tangu Zama za Manabii hadi karne ya makala hii.
Kumbukumbu zipo kuyathibitisha hayo, kwani hata yale mapambano makubwa ya mwanaharakati mashuhuri, Mohandas Gandhi yaliyoitwa ‘Satyagraha’ katika kuikomboa India kutoka katika makucha ya dhulma, yasingelinoga bila ya kuwepo maajabu ya mwanamama jasiri na mshairi maarufu wa bara hilo na kote duniani, Bi Sarojini Naidu.
Alitumia sauti na kalamu yake kuungana na juhudi kubwa isiyokuwa na madhara wala maafa ‘non-violence movement’, ambayo iliweza hata kuuweka rehani uhai wake, na hivyo kuidhihirishia dunia maajabu ya mwanamke jasiri ‘the majic of a strong woman’.
Halin Ibrahim Muhammed aliseema Wanawake wamehamasika kugombea nafasi mbali za kisiasa na.kiserikali ukilinganisha na wakati uluopita wanawake leo ni madhubuti.
Hii umetoka a na kupata mafunzo mbali mbali kutoka kwa mashirik yanayojali maslah ya mwanamke kwa maendeleo endelevu.
Bi Halima pia hakuacha kutoa ya moyoni dhidi ya changamoto na kueleza kuwa ushiriki wa mwanamke ktika maamuzi bado ni mdogo hali ambayo inakinzana na azma ya kujenga jamii isiyokuwa na ubaguzi kwa dira ya taifa.
“Vyama vyetu ambavyo hutumia kuelekea katika uongozi bado nako mifumo dume inaendelea kitu ambacho hawafanya wanawake wengi kurudi nyuma” alisema Halima.
Bi Halima ambaye aligombea Ubunge kwa tiketin ya Chama cha ACT wazalendo katika Jimbo la Mji |Mkongwe Visiwani Zanzibar alisema licha ya changamoto hizo harudi nyuma katika kupigania nafasi hiyo licha ya kushindwa kwa kile alichokieleza ana malengo makubwa kwa wanawake.
“Katika kupigania nafasi mwanamke katika taifa lazima wengine wajitolee muhanga kwa hiyo na mimi nataka niwe sababu ya mwanamke kufikia kule ambako tunataka” alisema Bi Halima.
Bi Halima alisema kukosekana kwa tume huru na Ruswaa katika nchi ya Tanzania ni sababu kubwa wanawake kukosekana kwa sauti ya mwanamke katika vyombo vya kutunga sharia.
Mwanasha Khamis Juma ambaye ni mwakilishi wa jimbo la Dimani kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) ametowa uzoefu wake wa uongozi na kusema licha ya chnagamako ziliopo mwanamke anaendelea kuja juu siku hadi siku.
Alisema kuwa tangu Zanzibar inapata wawakilishi wa kuteuliwa tuu lakini kwa sasa mpaka majimbo wanawake wamekuwa wakipambana na kuibuka vinara.
“Hii inaonyesha ni kiasi gani wanawake tunaweza kwa hiyo nakuombeni wanawake wenzangu tusikate tama” alisema Bi mwanaasha isha.
Aliwata wanawake kuacha kusikiliza maneno ya wanaume kwani alidai mara nyingi wanaume husema kuwa wanawake hawapendani.
“Hutumia neon hilo kutufanya kuwa dhaifu lakini sio kweli mwanamke rafiki yake ni mwanamke mwenzake tuu tusigombanishwe” alieleza Mwanaasha.
Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani alisema suala kuwa na Rais mwanamke Tanzania linawezekana hasa kutokana na uchaguzi uliopita wanawake wengine walijotokeza kugombea nafasi hiyo.
Na hivi tunavyokwenda Tanzania kuondoa mifumo kandamizi na kuwapatia wanawake nafasi ni dalili tosha kuwa siku moja Tanzania itakuwa na Rais mwanamke.
Mama Samia aaliwataka wanawake kushikana kisawasawa ili siku moja mwanamke katika nchi ya Tanzania awe kiongozi bora sana.
Mauwa Muhammed Mussa yeye ambaye amekuwa kijishuhulisha na siasa karibuni umri wake wote alisema licha ya mafanikio yoote yanayofikiwa juu ya mwanamke bado changamoto ni kubwa dhidi yao.
Alifahamisha kuwa Rasilimali fadha ni kikwanzo kikubwa kwao kushindwa kupata nafasi za uongoziu ambazo hugombewa.
“Utatakiwa kuweka mikutano au kampeni za nyumba kwa nyumba lakini huna fedha utafanyaje, huwezi hapo ndio wanaume hutuangusha, lakini tunauwezo wa kupambana kwa hoja” alisema Mauwa.
Alisema na changamoto nyengine Tanzania imekosa kuwa na misingi madhubuti ya kidemokrasia na kufanya wale ambao hugombea vyama vya uypinzania kunyimwa haki zao na kuonekana kama hawana haki ya kuwa viongozi wan chi.
Alisema pia nguvu kubwa ambayo hutumiwa na vyombo vya ulizi wakati uchaguzi ndio huwafanya wanawake wengi kurudi nyuma.
Bi Mauwa aliwaomba wanaharakjati kote duniani kuendelea na juhudi zao za kumjenga mwanamke kujiamini kwani hicho walikifanya leo mafanikio yake yanaonekana.
Mfano leo |baraza la wawakilishi lina wajumbe watano wa kuchaguliwa majimboni na hiyo ni dalili kubwa kuwa siku moja wanawake hasa Zanzibar watafika hatuia kubwa kama baadhi ya changamoto ambazo walizieleza wanawake zimeondolewa.
Katika kutoa shukrani katika hatua ambayo mwanamke amefika huwezi kuiacha Tasisi ya Tamwa Zanzibar katika kuwajenga uwezo wanawake na ujasiri.
No comments:
Post a Comment