Na Mwandishi Wetu
Mfuko wa hati fungani ni kati ya mifuko sita inayoendeshwa na Kampuni ya Serikali ya UTT AMS iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, mifuko mingine ni Umoja, Watoto, Wekeza Maisha, Ukwasi na Kujikimu.
Asili ya jina la mfuko huu, inatokana na kule unapowekeza, mfuko huu unawekeza kwenye kiwango kikubwa cha rasilimali zake kwenye hati fungani za serekali za muda mfupi na muda mrefu za serekali, amana za benki na kiasi kidogo kwenye hati fungani za kampuni binafsi.
Neno hati fungani lina maana ya mkopo kwa Serikali , Serikali hukopa kutoka kwa wananchi na taasisi zake ili kukidhi matumizi ya kila siku na ikiwa imefanya hivi tunasema serekali ime nadi hati fungani za muda mfupi, tunaposema muda mfupi tuna maanisha mkopo ambao hautazidi mwaka mmoja.
Mkopo unapokuwa wa muda mrefu tuna sema serikali imenadi hati fungani za muda mrefu na mkopo huu huwa ni kwa ajili ya maendeleo kwa mfano kujenga bara bara, reli, umeme na miradi mingine mikubwa kama maji, afya n.k , hati fungani hununuliwa kupitia benki kuu. Mkopeshaji anasema nimenunua hati fungani ya shilingi kadhaa ya miaka kadhaa.
Hati fungani za serekali, akaunti za muda maalumu za benki, na hati fungani za kampuni zote zina tabia moja kubwa. Kwanza ni uwekezaji ambao riba yake ni lazima iwe chanya, na muda wake lazima uwe unajulikana, mfano hati fungani ya miaka 20 kwa asilimia 15.49 ina maana kuwa utapatata aslimia 15.49 kwa kila mwaka kwa muda wa miaka 20. Na mgao wa pesa hizo huwa kila miezi sita maana ya ikiwa kila miezi sita unapata nusu ya asilimia 15.49 miaka ishirini ikiisha utapata pesa yako yote uliyo wekeza pamoja na riba, au kama wakati wa manunuzi kiasi cha mwisho hakikuwa na riba basi utapata ile pesa yako ambayo ulikuwa umewekeza.
Ukinunua hati fungani umeingia mkataba wa kuikopesha serekali, na ukiweka pesa kwenye akaunti za muda maalumu umeingia mkataba wa kuikopesha benki. Ndani ya mkataba huo huwezi kuongezea uwekezaji wako. Ukitaka kuongeza itakubidi ununue hati fungani nyingine, au ufungue akaunti ya muda maalumu nyingine. Pia uwekezaji huu ili upate faida nzuri unahitaji pesa nyingi, kuanzia shilingi 500,000 mpaka mabilioni. Ki kawaida kwa wale wenye kipato kidogo ni vigumu kuwekeza kwenye uwekezaji kama huu. Pamoja na ugumu huo ukivinja mkataba kuna adhabu zake. Japo kwa hati fungani unaweza ukauza kwenye soko la pili, na utauza kama kuna mtu anahitaji.
Ili kuondoa changamoto ya mtaji na muda. Uwekezaji wa pamoja kupitia mfuko wa hati fungani unatoa suluhisho, kupitia mfuko huu utafungua akaunti kuanzia shilingi 50,000 kiwango cha chini na utaendelea kuwekeza kuanzia shilingi 5,000 utawekeza mara nyingi uwezavyo na kiasi chochote uwezacho hapa basi utaona kuwa wenye kipato cha chini kabisa wanachanganyika na wenye kipato cha kati na cha juu kwa kuweka pesa zao kwenye mfuko mmoja halafu meneja-UTT anaziwekeza sehemu tofauti tofauti kwenye amana mbali mbalikama vile kwenye hati fungani za muda mfupi, akaunti za muda mfupi za mabenki, hati fungani za muda mrefu, akaunti za muda maalumu benki. Mwekezaji akihakishiwa kupata pesa zake muda wowote pale azitakapo bila kusubiri.
Kumbuka ungekuwa na shilingi 10,000; 50,000 usingeweza kufanya uwekezaji huu lakini kwa sababu umeungana na wenzako mmepata mabilioni ambayo yanawezesha kila mtu kufaidi matunda. Licha ya kupata pesa zako muda wowote, na kuwezesha wenye kipato cha chini kuungana na wenye kipato cha juu utaweza kuwekeza mara nyingi unavyoweza kupitia akaunti hiyo hiyo. Wingi wa pesa ndani ya uwekezaji wa pamoja utasaidia kuwekeza pesa nyingi zaidi kwenye akauti za muda maalumu kwenye banki. Kiasi cha faida yako kitategemea mtaji wako, lakini ki asilimia wawekezaji wote wanapata sawa.
Ukiwa kwenye uwekezaji wa pamoja, mfuko wa hati fungani una mipango tofauti, kuna mpango wa mwezi ambapo mwekezaji anapata gawio kila mwezi, pia uko mpango wa gawio kila baada ya miezi sita, na kama hutaki gawio kuna mpango wa kukuza mtaji. Na pia hakuna gharama za kujiunga wala kujitoa, unafuu wa kodi na faida nzuri kwa mwekezaji kulingana na mwenendo wa soko.
Uwekezaji kwenye hati fungani peke yake ni tofauti na Uwekezaji kwenye mfuko wa uwekezaji wa pamoja. Kwenye hati fungani peke yake hati fungani ya muda mrefu inalipa riba kubwa kuliko ya muda mfupi, mfano ya miaka kumi yaweza kuwa 11.44% wakati miaka 20 ni 15.49%. Pia ni lazima kufikiria uwezekano wa mkopaji kushindwa kulipa, na mara nyingi hii huwa kwa kampuni binafsi, ndiyo maana ni vizuri kuwekeza kupitia wataalamu kwani wao wana ujuzi na tathimini ni za umakini zaidi wao wataangalia uwezo wa mkopeswaji kulipa bila kukosa.
Lakini tukiwekeza kwenye mfuko wa uwekezaji wa pamoja tutakuwa tuko wengi, pia tutakuwa tumetawanya hatari za uwekezaji kwani hapa utakuwa ni mseto wa akaunti za mda maalumu, hati fungani za muda mfupi na muda mrefu, hati fungani za kampuni binafsi na bidhaa zingine za benki. Na mwisho wa siku unakuwa unapata mgao mara kwa mara mfano kwa mwezi wakati ingekuwa hati fungani pekee ingekuwa kila miezi sita.
Kwenye uwekezaji wa pamoja riba inaweza ikapanda au ikashuka kwa kutokana na mwendo wa soko la hati fungani lakini kwenye hati fungani kilicho kubaliwa ndiyo hicho hicho.
Kwa Makala hii tutakuwa tumeelewa umuhi wa mfuko wa hati fungani, na kwa wawekezaji wadogo au wenye kipato kidogo tumejifunza jinsi na nguvu ya kwenda pamoja. Na pia tuna weza ona umuhimu wa kutumia wataalamu kwenye kuwekeza. Pia tumejifunza kuwa kwenye kuwekeza kuna kupata kutoka kwenye riba tofauti tofauti, huku tukizingatia uwekezaji anuai.
Na ukumbuke kuwa ukiwekeza kwenye mfuko wa hati fungani, kazi ya usimamizi umemwachia meneja wakati wewe unaendelea na shughuli zingine, huumizi kichwa.
Jambo jingine ni sio lazima uchukuwe gawio, utaliancha lita changanyika na mtaji na vyote vitakupa faida. Utachukuwa hawio au sehemu ya uwekezaji wako au uwekezaji wako wote pale utakapo hitaji bila masharti, na bila gharama yeyote ile. Utajuwa thamani ya uwekezaji wako kila siku na utaona aidha ukipanda au ukishuka.
No comments:
Post a Comment