HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 01, 2021

SERIKALI YATENGA BILIONI 47 MIRADI YA MAJI BIHARAMULO

 


Naibu Waziri Wizara ya Maji, Merryprisca Mahundi, akimtua mama ndo kichwani kama ishara ya kuisogezea maji karibu jamii.

 

Na Alodia Dominick, Biharamulo

Serikali imetenga shilingi bilioni 47 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Katika bajeti ya mwaka 2021/2022.

Naibu Waziri wa Maji Merryprisca Mahundi amesema kuwa Katika bajeti ya mwaka 2021/2022 serikali imetenga bilioni 47 kwa ajili ya miradi ya maji fedha ambazo zitasaidia kukamilisha miradi iliyokwisha anza kujengwa.

Amesema kuna baadhi ya wakandarasi wamekuwa wakiomba tenda zaidi ya moja na kusababisha kukwamisha ujenzi wa miradi ya maji hivyo wakandarasi hawana budi kutenda mradi mmoja na kuumaliza kwa muda uliopangwa.

"Kuna wakandarasi ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya miradi zaidi ya mmoja na kushindwa kukamilisha kwa Wakati hakuna mkandarasi ataongezwa muda wa kumaliza mradi wa maji wajitahidi kumaliza kwa wakati"Amesema Mahundi

Amesema Lengo la Wizara ya maji ni kumtua mama ndoo kichwani na kuona muda waliokuwa wanatumia kuchota maji wanafanya shughuli za uzalishaji na wanafunzi waliokuwa wanatumia muda wao kwenda kuchota maji wanajisomea.

Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Biharamlo Lukas  Matina amesema kuwa serikali inatekeleza miradi sita katika wilaya ya Biharamlo kati ya miradi hiyo ambayo itagharimu bilioni 1 miradi mitatu imekamilika na mradi wa Kabindi ni miongoni mwa miradi hiyo ambapo ulianza kujengwa julai mosi, 2020 na unatarajiwa kukamilika desemba, 2021 na wananchi 18,031 katika vijiji vinne vya kata ya Kabindi ambavyo ni  pamoja na Kabindi, Nyamugogo, Chebitembe na Kikomakoma watanufaika nao.

Matina aliongeza kuwa, mradi huo umefikia 97% ya utekelezaji na shilingi 75 milioni zimeishatumika mradi utagharimu shilingi 235 milioni hadi kukamilika kwake.

Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Kabindi Dafroza Charles amesema kukamilika kwa mradi huo kutawapunguzia adha ya kusafiri zaidi ya kilomita tatu kwenda kufuata maji.

No comments:

Post a Comment

Pages