HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2021

WAZIRI MKENDA AZITAKA TAASISI ZA KIFEDHA KUTOA MIKOPO YA BEI NAFUU KWA WAKULIMA

 
Waziri wa kilimo, Profesa Adolf Mkenda akionyeshwa mkate uliokwa kwa unga wa viazi lishe na Mkurugenzi Mtendaji wa Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative (SUGECO), Revocatus Kimario wakati wa kuzindua mfumo wa Kizimba Business Model unaolenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara nchini mkoani Morogoro. wa kwanza kushoto ni Meneja wa benki ya NMB kanda ya mashariki, Dismas Prosper.Benki ya NMB ilishiriki kama mdau wa kilimo nchini.
 
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, akiangalia bidhaa za vyakula lishe vilivyozalishwa na Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative (SUGECO) kabla ya kuzindua mfumo wa Kizimba Business Model unaolenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara, mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki, Dismas Prosper. Benki ya NMB ilishiriki kama mdau wa kilimo nchini. (Na Mpiga Picha Wetu).
 
 
Na Ghisa Abby, Morogoro 

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amezitaka taasisi za fedha nchini kutoa mikopo yenye masharti nafuu ili kuwavutia vijana wenye nia ya kujikita kwenye kilimo biashara kupitia mfumo wa Kizimba Business Model (KBN) unaosimamiwa na Ushirika wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUGECO).

Profesa Mkenda amezinduka mfumo huo Machi 16,2021 mkoani Morogoro ambapo mbali na uzinduzi huo,amesema mfumo wa Kizimba utawezesha vijana wengi kujiunga pamoja kama ushirika na kutumia ardhi kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo kwa usimamizi wa wataalam wa taasisi hiyo. 

“Taasisi za kifedha hapa nchini nikutoa mikopo yenye riba nafuu ili waweze kuanzisha shughuli za kilimo kupitia mfumo huu wa kizimba ambapo utasaidia  kuongeza tija na uzalishaji mazao ya kilimo hali itakayochochea ukuaji wa ajira na kuongeza kipato,” amesema.

Amesema ili kukuza tija na uzalishaji kwenye sekta ya kilimo wizara yake itaendelea kuhamasisha kujengwa kwa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo bora na huduma za ugani hatua itakayokuza tija kwenye kilimo.

“Sekta ya kilimo inachangia chini ya theluthi moja kwenye pato la taifa ambayo ni asilimia 28 na kwa upande wa kilimo mazao bado mchango wake ni mdogo,"amesema.

Amesema takribani theluthi mbili ya nguvu kazi ya watanzania inajishughulisha na kilimo hivyo tafsiri yake ni kuwa tija bado ipo chini hivyo suala la kuongeze tija kwenye kilimo litasaidia ukuaji wa uchumi.

Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Raphael Chibunda amesema chuo hicho kitaendelea kushirikiana na wizara ya kilimo kusukuma na kubadilisha mfumo wa kilimo kuwa wa kibiashara ambapo sasa kiefanikiwa kuanzisha mashamba biashara kwenye maeneo yote ya chuo.

Amesema kuwa taasisi ya SUGECO inafanya kazi zake kwa kutoa mafunzo ya vitendo kupitia vitalu nyumba zaidi ya 100 kufundisha vijana stadi za kilimo biashara hatua inayochangia kukuza ajira na kipato kwa vijana.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Revocatus Kimario amesema mfumo wa kizimba Bussines Model ulizindiliwa utawezesha vijana wengi kukutana na wadau wa kilimo ikiwemo taasisi za fedha kwa ajili ya mitaji na wataalam wa ugani hatua itakayokuza uzalishaji wa mazao .

Kimario amesema Kizimba Bussiness Model unalenga kubadili fikra na mitizamo ya vijana kuhusu kilimo  ambapo itafanya waone kilimo ni ajira kama zilizvyo ajira zingine kupitia vikundi kwenye halmashauri ambapo kilimo vizimba itaanzishwa.

No comments:

Post a Comment

Pages