Kamati
ya Bunge ya Sheria Ndogo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo leo wamekubaliana kushirikiana katika kusukuma mageuzi katika
sekta ya filamu nchini.
Kamati hiyo leo ilikuwa ikisikiliza
maelezo ya Wizara ya Habari kuhusu maboresho katika Kanuni za Sheria ya
Filamu na maoni yaliyotolewa na wadau ili kuiimarisha tasnia hiyo.
"Sekta
ya filamu ni kubwa duniani na hapa nchini nikiwaangalia viongozi wa
sasa wa wizara naona kabisa wadau wakitoa ushirikiano na kuwa tayari kwa
mageuzi tutafika mbali," alisema Ridhiwani Kikwete, Makamu Mwenyekiti
wa Kamati hiyo ambayo leo aliongoza kikao hicho.
"Sisi kwa sasa
tumekubaliana kuongeza spidi katika utendaji wetu katika kuhakikisha
tunaleta mageuzi katika sekta hizi," alisema Waziri Innocent Bashungwa.
Katika
mageuzi ambayo yameshaanza kutekelezwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Dkt. Hassan Abbasi amesema tayari Serikali imeanzisha Mfuko wa Sanaa na
Utamaduni.
"Na Mfuko huu utakaokuwa mkombozi kwa wadau wetu wa
sanaa wakiwemo wale wa filamu umeshatengewa bajeti katika mwaka ujao wa
fedha. Kazi kwao wadau wetu, wajibu wao ni kuyaunga mkono mageuzi haya
ili twende pamoja," alisema Dkt. Abbasi.
March 29, 2021
Home
Unlabelled
WIZARA YA HABARI, KAMATI YA BUNGE WAKUBALIANA KUSUKUMA MAGEUZI TASNIA YA FILAMU
WIZARA YA HABARI, KAMATI YA BUNGE WAKUBALIANA KUSUKUMA MAGEUZI TASNIA YA FILAMU
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment