Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Bi. Tano Mwera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Wanawake Busega (Busega Women's Forum 2021) litakalofanyika 21 Aprili mwaka huu, ukumbi wa Silsosi Nyashimo
Jukwaa hilo mwakanhuu ni la msimu wa Nne tokea kuanzishwa kwake na Mkuu wa Wilaya ya Busega kwa ushirikiano na Benki ya CRDB.
"Tarehe 21 April 2021siku ya Jumatano, Kuanzia saa tatu Asubuhi mpaka saa kumi jioni Wajasiliamali wote mnakaribishwa kuja kuuza na kuonyesha bidhaa zenu ni bure kabisa. Kazi iendelee.
"Hii ni fursa ya kipekee kwa Wanawake wote kuja kwa wingi kujifunza mambo mbali mbali ya kibiashara na ujasiliamali.
Kikubwa ubebe na kitambulisho chako cha NIDA na kiasi cha Tshs 5000 kwa ajiri ya kufungua akaunti ya Malkia ya CRDB" Ilieleza taarifa hiyo.
Aidha katika jukwaa hilo, pia watatumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuanza Uongozi wake vizuri kuendeleza yale yaliachwa na watangulizi wake.
Kongamano hili pia linatarajiwa kuwa na huduma ya vyakula na vinywaji ambavyo vitatolewa bure kwa washiriki wote ambapo pia wanaweza kuwasiliana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya 0715367629
No comments:
Post a Comment