NA MWANDISHI WETU
KLABU
ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC), inampongeza Rais
Samia Suluhu Hassan kwa kuagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuvifungulia
vyombo vya habari vilivyofungiwa.
Pia
DCPC imefurahishwa na kauli ya Rais Samia kuwataka watendaji wa wizara
hizo kuacha kutumia mabavu wakati wa kufanya maamuzi badala yake watumie
kanuni na sheria zilizopo.
Sisi
DCPC tunaamini watendaji wa Wizara ya Habari ya Habari, Sanaa na
Utamaduni watayafanyia kazi kwa haraka maagizo ya Rais Samia na
kurejesha ajira za wanahabari na wafanyakazi wa idara nyingine
zilizopotea kwa kufungwa kwa vyombo vya habari.
DCPC tunaamini kwamba sasa uhuru wa vyombo vya habari uliominywa kwa miaka kadhaa sasa unarejea.
Pia tunaiona azma ya Rais Samia ya kuongeza mawanda ya ukusanyaji wa kodi na kusaidia katika kuleta maendeleo ya nchi.
Uamuzi
huu wa Rais Samia umekuja wakati muafaka kwani tasnia ya habari kwa
miaka mitano ilipita kwenye wakati mgumu hali ikiyosababisha kundi kubwa
la wanahabari mahiri na makini kukosa kazi.
DCPC
tunatoa wito kwa wanahabari kuendelea kufanyakazi zao kwa weledi na
kuzingatia sheria ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 na kanuni
za utangazaji ili kufanyakazi kwa amani kwa kuwa tasnia ya habari ni
mhimili wa nne wa dola.
No comments:
Post a Comment